1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Vita vya Israel-Hamas: Umaarufu wa Fatah wazidi kushuka

John Juma
7 Desemba 2023

chama kikubwa cha Wapalestina Fatah, kimekuwa kikipoteza umaarufu wake mnamo wakati vita vya Gaza vikiendelea.

https://p.dw.com/p/4Zt1P
Mahmoud Abbas, rais wa Mamlaka ya Palestina
Mahmoud Abbas, rais wa Mamlaka ya PalestinaPicha: Christophe Ena/AP/dpa/picture alliance

Wakati vita vya Israel na Hamas vikiendelea katika Ukanda wa Gaza, chama kikubwa cha Wapalestina Fatah, kimekuwa kikipoteza umaarufu wake katika eneo hilo ambako wanamgambo wa Kiislamu waliwatimua kwa nguvu waliokuwa wapinzani wa chama hicho mnamo mwaka 2007. 

Wakati kundi la Hamas lilichagua machafuko, chama cha Fatah kilichagua njia ya mazungumzo kufanikisha ahadi ya uundaji wa taifa la Palestina chini ya mikataba ya Oslo ya mwaka 1993. Hali hiyo imechangia umaarufu wa chama hicho kushuka.

Mashirika ya UN yashinikiza kwa pamoja usitishaji vita Gaza

Mahmud Abbas, amekuwa akiongoza Mamlaka ya Palestina iliyoundwa mwaka 1994 na ambayo ina sehemu ya udhibiti wa kiutawala katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Israel.

Lakini kwa sasa Mamlaka ya Wapalestina imedhoofika kuliko hapo awali, na migawanyiko ya kisiasa imezidi kuongezeka tangu vita vya Israel na Hamas vilipoanza Oktoba 7.

Blinken afanya ziara ya kushtukiza Ukingo wa Magharibi

Siku hiyo wanamgambo wa Hamas, kundi ambalo Israel, Marekani na Umoja wa Ulaya miongoni mwa nchi nyingine, zimeliorodhesha kuwa la kigaidi, walivuka mpaka na kufanya shambulizi baya la kushtukiza kusini mwa Israeli na kuua karibu watu 1,200, wengi wao wakiwa raia. Hayo ni kulingana na serikali ya Israeli.

Pia waliwashika mateka karibu watu 240 na kuwapeleka Gaza. Tukio hilo lilisababisha Israel kutangaza vita dhidi ya Hamas. Vikosi vya Israel vimekuwa vikifanya mashambulizi makali ya angani na ardhini kwa lengo la kuliangamiza Hamas na kuliondoa madarakani katika Ukanda wa Gaza.

Waandamanaji wajitokeza Ukingo wa Magharibi Novemba 30, 2023
Waandamanaji wajitokeza Ukingo wa Magharibi Novemba 30, 2023Picha: Issam Rimawi/Anadolu/picture alliance

Mgawanyiko wa maoni kati ya wazee na vijana

Wizara ya Afya ya Gaza inayodhibitiwa na Hamas, imesema zaidi ya watu 16,200 wameuawa kufuatia mashambulizi hayo, ikisema wengi wao wakiwa raia.

Wapalestina waandamana kulaani shambulio la hospitali Gaza

Wazee katika Ukingo wa Magharibi ambako chama cha Fatah kina wafuasi wengi, wanataka utulivu kuwepo ili mazungumzo yafanyike. Katika hali hiyo hawahatarishi msimamo na manufaa wanayofurahia chini ya Mamlaka ya Wapalestina.

Lakini kizazi cha vijana huko, kinasema hakina chochote cha kupoteza, na kinataka kufufua tawi la kivita la Fatah kiitwacho Brigedi za Mashahidi wa Al-Aqsa.

Zaidi ya yote, kikazi hicho kinataka kumaliza makubaliano ya ushirkiano wa kiusalama kati ya Mamlaka ya Wapalestina na Israel, ambayo wanahisi yanasaliti azma ya Palestina.

Afisa mmoja wa chama cha Fatah ambaye alizungumza na shirika la habari la AFP kwa sharti la kutotambulishwa, amesema viongozi ambao wanaweza kuwa na ushawishi wana maslahi mengi ya kibinafsi yanayohusishwa na Mamlaka ya Palestina, na hawawezi kuthubutu kuzungumza dhidi ya rais wake Mahmud Abbas.

Vita vya Israel dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza vimesababisha mgawanyiko wa maoni kuhusu chama cha Fatah
Vita vya Israel dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza vimesababisha mgawanyiko wa maoni kuhusu chama cha FatahPicha: Ahmed Zakot/Reuters

Shinikizo dhidi ya Rais Abbas

Kulingana na afisa mwengine wa Fatah ambaye pia hakutaka kutambulishwa, viongozi wa chama hicho wanachukua tahadhari wasionyeshe ishara yoyote ya kuunga mkono Hamas, kwa sababu ya shambulizi lake la Oktoba 7.

Abbas mwenye umri wa miaka 88, hana umaarufu katika Ukingo wa Magharibi ambako vita vya Israel na Hamas vimesababisha kuongezeka kwa uungwaji mkono kwa Hamas.

Mnamo Oktoba 17, polisi ya Mamlaka ya Palestina ilitumia mabomu ya kutoa machozi dhidi ya waandamanaji waliopaza sauti wakisema "Ondoka, wananchi wanataka rais ang'atuke.”

Israel yaimarisha usalama wakati wa maadhimisho ya kutekwa kwa Jerusalem

Kulingana na Xavier Guignard ambaye ni mchambuzi Mamlaka inazidi kuonekana kuafikiana na sera za Israel, kutokana na kutochukua hatua au kutokana na ushirikiano wake wa kiusalama.

Baada ya Abbas kumrithi mwanzilishi wa Fatah Yasser Arafat, aliyefariki mwaka 2004, wapiganaji wa Brigedi za Mashahidi wa Al-Aqsa waliwekwa kando.

Wengi wa wapiganaji wake walikuwa wameuawa katika mapigano, mashambulizi, au kufungwa na Israel, wengi walihukumiwa kula kalenda maisha.

Chanzo: AFPE