1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viwanja viwili vya ndege vyafungwa Ujerumani

25 Mei 2011

Eneo la kaskazini la bara la Ulaya linatarajiwa kuingia katika mtafaruku mpya wa safari za anga leo kutokana na jivu linalotoka katika volcano nchini Iceland. Viwanja viwili vya Ujerumani vimefungwa

https://p.dw.com/p/11NZW
Jivu likitoka katika volcano katika mlima nchini Iceland mwaka jana 2010.Picha: AP

Eneo la kaskazini la bara la Ulaya linatarajiwa kuingia katika mtafaruku mpya wa safari za anga leo kutokana na jivu linalotoka katika volcano nchini Iceland.

Deutschland Flughafen Vulkanasche
Wasafiri wakiwa wamekwama katika uwanja wa ndege wa mjini Duesseldorf, Ujerumani, mwaka jana kutokana na jivu linalotoka katika volcano.Picha: AP

Idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini Ujerumani imetangaza kuwa anga katika miji ya kaskazini ya Ujerumani litafungwa mapema leo Jumatano asubuhi kutokana na kiwango kikubwa cha majivu hewani kutokana na mlipuko wa volcano nchini Iceland. Maafisa wamesema jana Jumanne kuwa hakutakuwa na ndege itakayoruka ama kutua katika uwanja wa ndege wa Bremen, kuanzia saa 11 alfajiri leo ama katika uwanja wa ndege wa Hamburg, kuanzia saa 12 asubuhi leo Jumatano. Idara hiyo imesema kuwa inawezekana anga katika mji wa Berlin na Hannover likaathirika pia. Jana Jumanne, mamia ya safari za ndege katika anga la Uingereza zilifutwa wakati upepo ulisukuma mawingu ya jivu kutoka volcano ya Grimsvotn nchini Iceland na kuelekea kaskazini mwa Uingereza, hususan nchini Scotland.