1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vurugu zasababisha mauaji ya watu 12 Syria

7 Aprili 2024

Shirika la uangalizi wa vita nchini Syria limesema watu 12 wameuwawa Kusini mwa mkoa wa Daraa katika vurugu zilizosababishwa na mripuko uliotokea hapo jana na kusababisha mauaji ya kundi moja la watoto.

https://p.dw.com/p/4eWAN
Daraa
Mkoa wa Dara unaoathirika kwa vita SyriaPicha: Mohamad Abazeed/AFP/Getty Images

Daraa ndio lilikuwa chimbuko la maandamano ya mwaka 2011 dhidi ya utawala wa rais Bashar al Assad, lakini likarudi chini ya udhibiti wa serikali mwaka 2018 chini ya makubaliano yaliyosimamiwa na Urusi. 

Raisi: Iran italipa kisasi shambulio la ubalozi wetu Syria

Shirika hilo la Syria linaloangazia pia masuala ya haki za binaadamu katika maeneo ya vita limesema mtu aliyetambuliwa kama Ahmed al-Labbad anayeongoza kundi la wanamgambo, alituhumiwa na wapinzani wake kushambulia kwa kifaa alichokiripua katika mkoa wa Sanamayn na kusababisha mauaji ya watoto wanane, madai ambayo ameyakanusha.