1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vurugu zaua 20 nchini Misri

Admin.WagnerD2 Mei 2012

Zikiwa zimesali wiki tatu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa rais nchini Misri, vurugu zimetokea katika mji mkuu Cairo ambapo watu 20 wameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 160 kujeruhiwa.

https://p.dw.com/p/14oDf
Mapambano yakiendelea nchini Misri
Mapambano yakiendelea nchini MisriPicha: Reuters

Asubuhi ya Jumatano, mbele ya wizara ya Ulinzi ya Misri mjini Cairo kulishuhudiwa mshikemshike. Ndugu wa familia moja wanangua kilio mbele ya mwili wa ndugu yao uliyolala kwenye dimbwi la damu. "Oh Mungu wangu, hii ni damu ya ndugu yangu," anapiga yowe mwanaume moja.

Mwanaume huyo analia tena na tena . Kwa mujibu wa madaktari miili ya watu wanane imekutwa imekatwa korodani. Shahidi moja amesema, baadhi ya wavamizi wameua hata watu waliyokuwa wanafanya ibada.

Wauaji hao inasemekana walijipenyeza miongoni mwa wandamanaji waliyokuwa wanandamana kupinga kuenguliwa kwa mgombea wao, Hasem Abu Ismail, mwanaharakati wa Salafi kwa madai kuwa alikuwa na uraia wa nchi mbili kinyume na matakwa ya kisheria.

Wandamanaji wakirusha mawe.
Wandamanaji wakirusha mawe.Picha: Reuters

Vurugu hizi ambazo ziliendelea wakati wote wa asubuhi kabla ya kupungua mida ya mchana, zimetia doa jitihada za nchi hiyo kueresha utulivu na kuelekea kwenye demokrasia ya kweli. Wakati vurugu hizo zikiendelea, sauti zilikuwa zikisikika zikiuliza wapi walipo wanajeshi.

Mabomu ya kinyeji yatumika
Vijana waliyojawa na hasira walikuwa wakipiga kelele za kuupinga utawala wa kijeshi huku wakirusha mawe na mabomu yaliyotengenezwa kienyeji kwa kujaza petroli kwenye chupa na kisha kuzirusha. Shahid moja aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa aliwaona baadhi ya watu wakiwa wamebeba silaha na mmoja alikuwa na kitara.

Jeshi lililaazimika kutuma magri mengine na kuongeza vikosi lakini liliahidi katika taarifa yake kuwa lisingeingilia kuzuia mandamano ya amani, lakini lilweka vuzuizi kuelekea makao makuu ya wizara ya uslinzi ikiwa ni pamoja na senyenge, na wanajeshi waliojiandaa kukabiliana na fujo.

Parlament in Ägypten setzt aus Protest gegen Militärrat Arbeit aus Wafuasi wa Hazem Abu Ismail wakiswali nje ya Wizara ya Ulinzi nchini Misri.
Wafuasi wa Hazem Abu Ismail wakiswali nje ya Wizara ya Ulinzi nchini Misri.Picha: AP

Mandamano pia yalitangulia uchaguzi wa wabunge Novemba mwaka jana. Chama cha udugu wa Kiislam ambacho kinadhibiti mabunge yote mawili ya Misri, kimetishia kussusia mkutano ulioitishwa na watawala wa kijeshi wenye lengo la kutafuta ufumbuzi wa mgogoro uliopo kati ya Bunge na serikali ya muda inayoungwa mkono na jeshi.

Chama cha Uhuru na Haki ambacho ni tawi la kisiasa la Udugu wa Kiislam kilisema vurugu hizi ni njama ya wanajeshi kutaka kukataa kukabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia na mgombea wake, Mohamed Mursi alisema hataendesha kampeni kwa muda wa siku mbili ili kuomboleza vifo vilivyotokea.

Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga\RTRE
Mhariri: Mohammed Abdul Rahman.