1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vyama vya upinzani kuunda serikali ya mseto Pakistan

22 Februari 2008
https://p.dw.com/p/DBS3

ISLAMABAD:

Vyama viwili vikuu vya upinzani vilivyopata ushindi mkubwa katika uchaguzi nchini Pakistan,vinatazamia kuunda serikali ya mseto.Waziri Mkuu wa zamani Nawaz Sharif amesema,chama chake cha Muslim League-N na PPP cha waziri mkuu wa zamani Benazir Bhutto alieuawa mwezi wa Desemba,vimekubali kushirikiana. Chama cha PPP kinachoongozwa na mjane wa Bhutto,Asif Ali Zardari,kilijinyakulia ushindi mkubwa katika uchaguzi wa siku ya Jumatatu na hivyo kitashika wadhifa wa waziri mkuu.

Ushirikiano wa vyama hivyo viwili vilivyokuwa mahasimu hapo zamani,ni changamoto kali kwa Rais Pervez Musharraf.Kwa mara nyingine tena kiongozi wa chama cha PPP amemtaka Musharraf aondoke madarakani.Mwaka jana Musharraf aliwahamakisha Wapakistani wengi alipotangaza hali ya hatari.