1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vyama vya upinzani nchini Malaysia vyaunda muungano.

1 Aprili 2008
https://p.dw.com/p/DYaH

Kuala Lumpur.

Vyama vya upinzani nchini Malaysia vimekubaliana kuunda muungano rasmi. Kiongozi wa upinzani Anwar Ibrahim amewaambia waandishi wa habari leo kuwa muungano huo utajumuisha chama chake pamoja na makundi ya kihafidhina ya vyama vya Kiislamu na chama cha watu wenye asili ya China.

Hatua hiyo ina lengo la kuimarisha nafasi ya vyama vya upinzani kwa wananchi ikiwa ni nguvu mbadala kwa chama tawala.

Vyama vikuu vitatu vya upinzani vimeshinda idadi kubwa ya viti bungeni katika uchaguzi mkuu wa bunge March 8, na kusababisha kuporomoka kwa nguvu za chama tawala cha National Front Coalition kwa mara ya kwanza katika historia yake ya miaka 50 ya utawala.