1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vyama vya vyombo vya habari vyasimamishwa kazi Sudan Kusini

John Juma
2 Novemba 2017

Wakala unaosimamia vyombo vya habari Sudan Kusini umevisimamisha kazi vyama vyote vya vyombo vya habari nchini humo

https://p.dw.com/p/2muBV
Südsudan Leser der Zeitung 'Juba Monitor'
Picha: Getty Images/AFP/S. Bol

Wakala unaosimamia vyombo vya habari Sudan Kusini umevisimamisha kazi vyama vyote vya vyombo vya habari nchini humo wakati vikisajili kupata lesini za kuendesha shughuli zao. Waandishi habari wamesema hayo, huku hatua hiyo ikisababisha wasiwasi kuhusu uwezekano wa kuviandama vyombo huru vya habari.

Muongozo uliotolewa kwa vyama vitatu vya wandishi habari vya Sudan Kusini wiki hii na nakala kulifikia Shirika la habari la Reuters jana, umewapa siku 7 kuhakikisha vinapata leseni au kukabiliwa na hatari ya kufungiwa moja kwa moja.

Si maafisa wa wizara ya habari wala wakala wa mawasiliano wa taifa walioweza kupatikana mara moja.