1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vyombo vya habari vyazuiliwa visiripoti habari

28 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CTz2

Meya wa mji wa Mogadishu, Mohamed Omar Habeb, amevipiga marufuku vyombo vya habari nchini Somalia visiripoti habari kuhusu wanamgambo, harakati za kijeshi na wakaazi wa Mogadishu wanaoukimbia mji huo unaokabiliwa na machafuko.

Hayo yamesemwa na kundi moja linapigania haki za binadamu nchini Somalia, SOHRIDEN.

Amri ya meya huyo wa Mogadishu inazuia habari zisitoke Mogadishu, ambako waandishi wa habari na vyombo vya habari vinalengwa na vikosi vya Ethiopia na serikali ya mpito ya Somalia pamoja na wanamgambo ambao wamekuwa wakipigana tangu mwezi Januari mwaka huu.

Waandishi wa habari wasiopungua wanane wameuwawa na wengine kadhaa kutiwa mbaroni, kushambuliwa au vifaa vyao kuibiwa, hivyo kuifanya Somalia kuwa nchi ya pili hatari duniani kwa waandishi wa habari baada ya Irak.