1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandamanaji wakataa kubakia majumbani

P.Martin29 Septemba 2007

Licha ya hatua kali za utawala wa kijeshi,mamia ya watu nchini Myanmar hii leo walikusanyika mjini Yangon.

https://p.dw.com/p/CH7T
Waandamanaji wakidai demokrasia nchini Myanmar
Waandamanaji wakidai demokrasia nchini MyanmarPicha: AP

Juma hili jumuiya ya kimataifa ilihamakishwa baada ya watawa na raia waliokuwa wakiandamana kufyatuliwa risasi.Si chini ya watu 13 waliuawa na mamia wengine wametiwa ndani.

Hii leo,mjumbe wa Umoja wa Mataifa,Ibrahim Gambari amewasili nchini Myanmar kuzungumza na viongozi wa kijeshi.Lengo ni kuishawishi serikali hiyo,kukomesha matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji wanaogombea demokrasia.

Katika mji mkuu wa Ujerumani,Berlin kiasi ya watu 200 walikusanyika mbele ya ubalozi wa China, katika ishara ya kuwaunga mkono waandamanaji nchini Myanmar.China ni mshirika muhimu wa Myanmar.