1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandamanaji wapambana na polisi Ugiriki

19 Oktoba 2011

Ugiriki, waandamanaji wamepambana na polisi mbele ya jengo la bunge mjini Athens baada ya maelfu ya watu kukusanyika eneo hilo ili kuanzisha mgomo mkuu nchini kote, kuupinga mpango mpya wa kubana matumizi serikalini.

https://p.dw.com/p/RroN
epa02972027 Protesters clash with riot police during a general strike demonstration in Athens on 19 October 2011. Protesters oppose strict austerity measures imposed by the Greek government and troika. Greek riot police fired tear gas and clashed with anti-austerity demonstrators as more than 100,000 protesters were converging on the country_s parliament in central Athens. EPA/ORESTIS PANAGIOTOU +++(c) dpa - Bildfunk+++
Mapambano yamechafua maandamano ya mgomo mkuuPicha: picture-alliance/dpa

Kwa mara ya kwanza kabisa tangu mzozo wa Ugiriki kuibuka miaka miwili iliyopita, waandamanaji leo wamejipenyeza hadi kwenye ngazi za jengo la bunge. Waziri Mkuu George Papandreou aliepoteza umaarufu wake, ametoa mwito kwa wananchi wake kuziunga mkono hatua mpya za kubana matumizi. Miongoni mwa hatua hizo, ni kupandisha malipo ya kodi, kushusha mishahara na kupunguza idadi ya wafanyakazi katika sekta ya umma. Waandamanaji wenye hasira na waliyochoshwa na mipango ya kubana matumizi mara kwa mara, wamekusanyika kwa maelfu kwenye Uwanja wa Syntagma katikati ya mji mkuu Athens kuanzisha mgomo mkuu wa siku mbili.

Media workers protest in central Athens, on Tuesday, Oct. 18, 2011. Greek railway workers and journalists joined ferry crews, garbage collectors, tax officials and lawyers on Tuesday in a strike blitz against yet more austerity measures required if the country is to avoid defaulting on its debts.(Foto:Petros Giannakouris/AP/dapd
Wagiriki wamechoshwa na mipango ya mara kwa mara kubana matumiziPicha: dapd

Polisi waliokuwa wakililinda jengo la bunge wametumia mabomu ya kutoa machozi baada ya polisi hao kushambuliwa na waandamanaji kwa mawe na mabomu ya petroli. Zaidi ya polisi 7,000 wametawanywa barabarani kuzuia machafuko. Hata hivyo maandamano hayo yametumiwa na makundi madogo ya wafanya ghasia kufanya uharibifu mbele ya hoteli za anasa na maduka makubwa. Katika mji mkubwa wa pili Thessaloniki, kiasi ya waandamanaji 100 wameshambulia makao makuu ya serikali ya mkoani na watu kadhaa wamejeruhiwa.

Mapamabano yaliyotokea, yametia doa mgomo uliyosababisha idara za serikali na maduka kufungwa na kusitisha huduma za kijamii. Kiasi ya safari za ndege 159 zimefutwa. Kwa mujibu wa polisi, zaidi ya watu 125,000 wanaandamana kote nchini humo, kuupinga mswada mpya wa kupunguza matumizi unaojadiliwa bungeni kabla ya sehemu ya mpango huo kupigiwa kura baadae leo hii. Kura ya pili kuhusu vipengele maalum, itapigwa kesho Alkhamisi.

Protesters shout slogans during a demonstration in the northern port city of Thessaloniki, Greece, Wednesday, Oct. 5, 2011. Greek civil servants walked off the job on a 24-hour strike Wednesday, paralyzing the public sector in a protest over ever-deeper austerity measures applied as the government struggles to avoid a catastrophic default. At least 10,000 protesters converged in Thessaloniki, and a crowd of about 16,000 gathered in the Greek capital. (Foto:Nikolas Giakoumidis/AP/dapd)
Mgomo mkuu umekwamisha sekta ya jamiiPicha: dapd

Viongozi wa kimataifa, wanaotoa msaada wa fedha kwa Ugiriki, wanapoteza subira na kuzorota kwa mchakato wa mageuzi wa serikali ya nchi hiyo, ambayo haikutekeleza malengo ya kudhibiti bajeti yake. Sauti zinazidi kupazwa kuitaka serikali ya Ugiriki iwe chini ya usimamizi mkali wa Umoja wa Ulaya ili kuhakikisha kuwa itawajibika kutekeleza mageuzi yanayohitajiwa.

Mwandishi: Martin,Prema/rtre

Mhariri: Yusuf Saumu