1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandamanji nchini Libya wavamia wizara ya sheria ya nchi hiyo.

Admin.WagnerD30 Aprili 2013

Waandamanaji waliobebe silaha nchini Libya wameizingira wizara ya Sheria ya nchini hiyo,wakidai maoafisa wa wizara hiyo waliokuwa na mafungamno na Muammar al-Gaddafi watolewe katika wizara hiyo

https://p.dw.com/p/18Prd
Waziri mkuu wa Libya Ali Zeidan
Waziri mkuu wa Libya Ali ZeidanPicha: AFP/Getty Images

Akizungumza na shirika la habari la AFP kiongozi wa wizara ya Habari nchini Libya Walid Ben Rabha,amesema kuwa waandamanji hao wametoa sharti la kuondoalewa wafanyakazi wa wizara hiyo na wizara kufungwa.

Kwa upande wao wandamanaji hao wamesema kuwa wataendelea kuzingira eneo hilo hadi hapo madai yao yatakapopigiwa kura na kupitishwa katika Bunge la nchi hiyo.

Bunge la Libya linausoma mswada huo wa sheria wa kuwatoa serikalini na katika nafasi za kisiasa wafanyakazi wote waliokuwa wanafanya kazi na utawala wa wa aliekuwa kiogozi wa nchi hiyo Muammar al-Gaddafi

Mswada huo iwapo utapitishwa,unaweza kuwaathiri viongozi wakubwa katika serikali ya Libya na kuunda matabaka ya kisiasa katika serikali .

Mwezi Machi mwaka huu waandamanaji hao walilizingira jengo la Bunge na kusababisha hali ya taharuki kwa kwa wabunge waliokuwa ndani ya jingo hilo kwa masaa kadhaa,wakitaka kupitishwa kwa sheria hiyo.

Bunge la Libya lililazimika kusimasiha vikao vyake kufuatia taarifaya kufungwa wizara ya mambo ya nje ya Jumapiliiliopita. Bunge hilo lilikuwa linatarajia kujadili sheria ya kutengwa kisiasa ambayo inatakiwa na wanamapinduzi hao wa Libya.

Madai ya wanamaandamano hao ni kutaka Bunge la Libya lipitishe sheria mpya ambayo itawatoa katika nafasi zao wafanyakazi  na mabalozi wote waliokuwa na mafungamno na utawala wa Muammar al-Gaddafi.

Maandamano hayo ya wanamapinduzi yanakuja wakati waziri mkuu wan chi hiyo Ali Zidan akionya kuhusu suala hilo na kusema kuwa serikali itajibu mashambulizi dhidi ya  watu hao wenye silaha.

Waandamanji nchini Libya
Waandamanji nchini LibyaPicha: Reuters

Hata hivyo inaelezwa kuwa baada ya waandamanji hao kuondoka katika Bunge la nchi hiyo,baadhi ya watu wenye silaha waliuvamia msafara wa magari ya spika wa bunge hilo Mohammed Megaryef,lakini hakukutokea athari yoyote.

Waandamanaji wamejaribu pia  kuivamia Wizara ya mambo ya ndani na Televisheni  ya taifa na kukwamisha  shughuli za wizara na kituo hicho cha habari.        

Serikali ya Libya kwa sasa inakabiliwa na changamoto za kisiasa kutoka kwa waasi walioshiriki katika mapambano ya kumuondoa madarakani Kanali  Muammar al-Gaddafi mwaka  2011,ambao wanaishikilia sehemu kubwa ya nchi hiyo.

Mwandishi:Hashim Gulana/AFP/DPA

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman