1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandishi habari wawili wauwawa Marekani

27 Agosti 2015

Aliyekuwa mwandishi habari za runinga ambaye aliwaua waandishi habari wawili wakati wa matangazo ya moja kwa moja huko Virginia kabla ya kujiua alikuwa ameonya juu ya kuwa na hamu ya kuua.

https://p.dw.com/p/1GMoA
WDBJ7 - Erschossene Journalisten Alison Parker und Adam Ward
Waandishi habari waliouwawa Alison Parker na Adam WardPicha: picture-alliance/AP Photo/ WDBJ-TV7

Aliyekuwa mwandishi habari za runinga ambaye aliwaua waandishi habari wawili wakati wa matangazo ya moja kwa moja huko Virginia kabla ya kujiua alikuwa ameonya juu ya kuwa na hamu ya kuua.

Mtu huyo Veste Lee Flanagan mwenye umri wa miaka 41 anayefahamika pia kama Bryce Williams alichapisha picha za mauwaji hayo kwenye mtandao.

Ripota Alison Parker mwenye umri wa miaka 24 na mpiga picha Adam Ward 27 walipigwa risasi wakati wakiendelea na maojiano yaliyokuwa yakipeperushwa moja kwa moja kwenye kituo cha televisheni cha WDBJ Kinachohusiana na Televisheni ya CBS huko Roanoke karibu kilomita 385 kusini mashariki mwa mji wa Washington

Haikuwa imebainika ikiwa muuwaji huyo alimfahamu Parker kabla ya mauwaji hayo kutokea.

Kauli ya rais Obama

Rais Barak Obama wa Marekani amesema kisa hicho cha kupigwa risasi na kuuawakwa waandishi habari ni cha kuvunja moyo.

Obama American University Rede
Rais Barack Obama wa MarekaniPicha: Reuters/J. Ernst

"Ninavujwa moyo kila mara ninaposoma na kusikia kuhusu visa kama hivi.Obama amesema.Amesema idadi ya watu wanaoaga dunia kutokana na visa vinavyohusiana na kupigwa risasi katika nchi hiii vinashinda vifo vinavyotokana na ugaidi.

Familia ,marafiki na jamii nzima wanaomboleza mkasa huo huku kisa hicho kiikibua mwito wa kudhibiti bunduki nchini humo.Flanagan anasemekana kuwa alikuwa amenunua bunduki yake kihalali.

Mauwaji hayo yamezidisha mizozo ya bunduki nchini Marekani na kusababisha ikulu ya White House kutoa mwito wa hatua zichukuliwe na ikashangaa ni jinsi gani mtandao unavyotoa habari na haswa nafasi ya kuelezea uhalifu mbaya.

Picha za mkasa wa kutisha

Picha za video za kutisha zilizooyesha tukio hilo yaaminika zilichapishwa na Flagan mwenyewe kwenye mitandao ya twitter na Facebook.Hata hivyo picha hizo ziliondolewa baadaye

Wakati wa kisa hicho,mwandishi alliyeuawa Parker alikuwa akimhoji Vicki Gardner msimamizi wa chama cha wafanyabiashara cha Smith Mountain Lake kando ya mto katika hoteli ya Bridgewater Resort kwenye mji wa Moneta karibu na Roanoke.

Sauti za risasi zilisikika,na vilio huku camera ya Ward ikianguka sakafuni, na kuonyesha mtu aliyekuwa na bunduki akilenga bunduki yake chini.

Kuna uwezekano hawakumuona mtu huyo aliyewapiga risasi.Kulingana na video hiyo,baada ya kelele hizo kuanza kusikika ,Parker anaonekana akikimbia.Mkono wa muuwaji huyo unaonekana vizuri akiwa amevalia shati yenye mistari ya rangi mbalimbali.

Gardner,aliyekuwa akihojiwa amekuwa hospitalini katika hali thabiti katika hospitali ya Roanoke.

Shirika la habari la ABC limesema lilipokea waraka wa kurasa 23 kutoka kwa mwanamme anayejitambulisha kama Bryce Williams karibu saa mbili baada ya tukio hilo.Mwanaume huyo alipiga simu akisema amewapiga risasi watu wawili huku akiarifu kuwa anasakwa na maafisa wa polisi kila mahali ,kabla ya simu yake kukatika kulingana na ABC.

Katika waraka wake Flanagan mmarekani mweusi aliyefutwa kazi 2013 na kituo cha televisheni cha WDBJ alisema alipata kichaa kutokana na kisa cha mwezi Juni ambapo wamarekani wengi weusi waliuawa kanisani huko South Carolina. Flagan pia analalamikia kile alichokiita"arifa ya kujiua kwa marafiki na familia"inayoelezea kuwa ubaguzi wa rangi kwa kukejeliwa kwa kuwa shoga mweusi."Itaonekana mimi nimekasirika lakini ni kweli nimekasirika kwani nina haki ya kukasirika.Lakini nitakapoondoka ulimwengu huu ninataka niwe na amani moyoni". Waraka huo ulielezea.

Meneja wa kituo hicho cha televisheni kwa jina Marks, amesema Flanagan alifutwa kazi baada ya kuhusika katia visa vilivyotokana na Jazba zake

Mwandishi:Bernard Maranga/AP/AFP

Mhariri:Yusuf Saumu