1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanahusishwa na jaribio la mapinduzi

31 Oktoba 2016

Polisi Uturuki inawashikilia waandishi wa habari na mhariri mkuu wa gazeti pinzani la Cumhuriyet huku ikitoa waranti wa kukamatwa kwa maafisa wengine, wakihusishwa kuchochea jaribio la mapinduzi la Julai mwaka huu.

https://p.dw.com/p/2RvYn
Türkei Cumhuriyet Chefredakteur festgenommen
Picha: Getty Images/AFP/O. Kose

Mwendesha mashitaka katika mji wa Instanbul anawashutumu wafanyakazi wa gazeti hilo kwa kufanya makosa kwa niaba ya makundi ya kigaidi kwa kuchapisha habari ambazo zilihalalisha jaribio hilo ambalo hata hivyo halikuwafanikiwa.

Gazeti la Cumhuriyet ambalo  mwaka huu lilishinda tuzo ya haki ya kuishi inayojulikana kama tuzo mbadala ya Nobel, mwaka jana pia lilishinda tuzo iliyotolewa na shirika la waandishi wa habari wasio na mipaka.

Katika mtandao wake, gazeti hilo limethibitisha kuwa mhariri mkuu wa Gazeti hilo Murat Sabuncu na mchambuzi  Guyar wanashikiliwa na polisi baada ya kukamatwa katika nyumba zao,  na kuongeza kuwa wengine wanne wanashikiliwa pia. Pia limesema kuwa polisi imezuia kuwasiliana na wanasheria na hivyo wataendelea kushikiliwa kwa muda wa siku tano

Gazeti hilo kwa upande wake linasema kuwa uamuzi uliochukuliwa ni mapinduzi dhidi ya democrasia, mhariri mkuu wa zamani wa gazeti hilo Can Dandur ambaye kwa sasa anaishi nchini Ujerumani alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kufuatia kuchapisha habari ambayo ilikuwa inalishutumu jeshi la uturuki kupenyeza silaha kwa waasi nchini Syria.

Türkei | Recep Erdogan bei der Eröffnung der High Speed Train Station in Ankara
Rais wa Uturuki Recep ErdoganPicha: picture-alliance/abaca

Kuchapishwa kwa habari hiyo kulimfanya Rais wa Uturuki Recep Tayip Erdogan kusema na ameendelea kusema kuwa Dandur atalipa gharama kubwa kwa kuandika ripoti hiyo, Dandur alikuwa akitafutwa kwa ajili ya kuulizwa maswali na nyumba yake uliyoko instanbul kufanyiwa ukaguzi

Uturuki hivi ssasa imetangaza hali ya hatari kufuatia jaribio la mapinduzi lililoongozwa na jeshi, katika miezi ya hivi karibuni vyombo vingi vya habari vimefungiwa na maelfu ya wafanyakazi wa umma kufukuzwa kazi na wengine 35,000 kukamatwa, sheria hiyo ya hali ya hatari inaipa serikali mamlaka mengi na kuzuia makundi ya kiraia mambo kadhaa ikiwemo kupata msaada wa kisheria.

Mwanasheria wa Diyarbakir ambaye ni meya mshirika hivi karibuni amelaani kitendo hicho kwa kusema

"Hata huko katika magereza ambako wamewapeleka itakuwa ni ujinga kukaa na kusubiri kuona haki inatendeka, kuwa wakweli hatukutegemea hivyo, haya sio maamuzi yamepitishwa kisheria, hii inaweza kuelezwa kuwa ni maamuzi ya kisheria"

Kufungwa kwa vyombo vya habari kama vile magazeti na televisheni kunalenga sana vyombo ambavyo vinashutumiwa kuwa na uhusiano na Fethulla Gulen, imamu wa kuturuki ambaye anaishi nchini Marekani ambaye Serikali ya nchi hilo imemshutumu kuhusika na jaribio hilo, idadi kubwa ya taasisi za habari za kikurd pia zimefungwa.

Mwandishi: Celina Mwakabwale/AP/dpa

Mariri:  Yusuf Saumu