1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti ya 2008

Abdulrahman, Mohamed12 Februari 2008

Ripoti ya mwaka ya shirika la waandishi wasio na mipaka imelaumu vikali ukosefu wa kuwajibika, undumila kuwili na uwoga wa baadhi ya nchi za magharibi na mashirika makubwa duniani, ambayo imesema zinahatarisha uhuru wa

https://p.dw.com/p/D6ac
Ripoti ya 2008


Kiongozi wa shirika hilo la waandishi wasio na mipaka  lenye makao yake mjini Paris Ufaransa  Robert Menard shirika ambalo hujulikana pia kwa kifaransa kama Reporters Sans Frontiers (RSF) amesema kwamba  alisema kutowajibika kwa baadhi ya  magharibi na   mashirika makubwa duniani ndiko kunakouhujumu na kuuathiri uhuru wa vyombo vya  habari . Akaongeza katika taarifa yake kwamba ukosefu wa moyo thabiti wa nchi za kidemokrasi, katika kutetea maadili ambayo wanapaswa kuyasimamia ni jambo linalotisha.


Bw Menard  hasa alililenga baraza la  haki za binaadamu la umoja wa mataifa lenye makao yake makuu mjini Geneva Uswisi, ambalo amedai lisalimu amri mbele ya mbinyo kutoka nchi kama Iran na Uzbekistan, wakati huo huo akikosoa udhaifu wa umoja wa ulaya kuelekea madikteta ambao hawakushtushwa hata na  kitisho cha vikwazo kutoka nchi za Ulaya.


Ripoti ya shirika hilo la waandishi wasio na mipaka kwa mwaka huu wa 2008 pia inatanabahisha juu ya kitisho kinacho wakabili waandishi habari kuanzia katika suala la usalama wao katika maeneo ya mizozo pamoja na  uchujaji wa  habari na vyombo vya habari kwa jumla hasa panapohusika na  matatizo yanayohusiana na  uchaguzi katika nchi mbali mbali mwaka huu.


Aidha imezingatia pia uchunuguzi juu ya uhuru wa vyombo vya habari katika kila   kanda duniani kwa mwaka 2007 na pia kurasa za  maelezo ya hali katika nchi 98.


Inataja kwamba  uwezekano wa waandishi kushambuliwa wakati wa  chaguzi zijazo huko Pakistan, Urusi, Iran na Zimbabwe ni mkubwa na kuna hofu kubwa ya kuandamwa katika mwaka huu 2008.

Suala jengine linalozingatiwa katika ripoti ya  shirika hilo la waandishi wasio na mipaka ni wasi wasi  juu ya usalama wa waandishi wanaoripoti  juu ya mizozo katika  nchi kama Somalia na Sri Lanka hadi Irak na maeneo ya Wapalestina.


Kuchujwa kwa vyombo vipya  vya habari ni kitisho kingine kinachozingatiwa  ikitajwa China ikiwa ni hatua zinazochukuliwa kabla  ya  michezo ya  Olimpik ya majira ya joto itakayofanyika Beijing mwaka huu.

Ripoti imesema hakuna  shirika lolote mbali na  kamati ya olimpik ya kimataifa linaloamini kwamba serikali ya China itapiga hatua ya maendeleo fulani ya maana kabla ya michezo hiyo kuanza,kwani  kila anapoachiwa huru mwandishi mmoja mwengine huingia gerezani.