1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandishi wawili wa habari watekwa nyara Irak

12 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D6OL

Waandishi wawili wa habari wa shirika la habari la CBS hawajulikani waliko katika eneo la kusini mwa Irak.

Habari ambazo hazijathibitishwa zinaashiria waandishi hao walitekwa nyara na genge la watu wapatao kumi katika hoteli moja ya mjini Basra juzi Jumapili.

Muungano wa waandishi wa habari nchini Irak umewatolea mwito watekaji nyara wanaowazuilia waandishi hao wawili wanaume wa shirika la CBS wawaachie huru.