1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandishi wawili wa habari watekwa nyara Irak

12 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D6ZC
Mwandishi habari raia wa Uingereza pamoja na mkalimani wake muirak wametekwa nyara katika mji wa Basra, kusini mwa Irak. Wote wawili wanalifanyia kazi shirika la habari la kimarekani la CBS. Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari nchini Irak waandishi hao wa habari walitekwa nyara karibu na hoteli yao kusini mwa mji wa Basra unaomilikiwa na waislamu wa madhehebu ya shia. Shirika la habari la CBS halijatangaza majina wa waandishi hao likisema hatua hiyo itayahatarisha maisha yao. Hapo jana mateka wawili wa kishia waliachiwa huru mjini Basra baada ya watekaji nyara kulipwa kitita cha pesa walichodai. Jeshi la Uingereza liliondoka kutoka mji huo wa mafuta ulio katika ghuba ya uajemi mwishoni mwa mwaka jana na kuliachia jeshi la Irak jukumu la usalama.