1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waangalizi wa EAC Kenya na Kinagaubaga

Saumu Ramadhani Yusuf19 Februari 2013

Wakati Kenya ikijiandaa kushiriki uchaguzi Machi nne mwaka huu. Waangalizi kutoka makundi mbali wameanza kuwasili nchini humo likiwemo la Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

https://p.dw.com/p/17h5p
The eight Kenyan presidential aspirants Mohammed Dida, James Ole Kiyiapi, Uhuru Kenyatta, Peter Kenneth, Musalia Mudavadi, Martha Karua, Kenyan Prime Minister Raila Odinga and Paul Muite (L-R) face off in the first ever presidential debate at Brookhouse School in Kenya's capital Nairobi February 11, 2013. The presidential television debate - the first ever held in the country - failed to produce a clear winner, but gave an early taste of what is expected to be a highly charged contest to run East Africa's economic powerhouse. Picture taken February 11, 2013. REUTERS/Stringer (KENYA - Tags: ELECTIONS POLITICS)
Mdahalo wa wagombea uraisPicha: Reuters

Jumuiya ya Afrika Mashariki wiki hii imetuma ujumbe wake wa waangalizi ukiongozwa na aliyekuwa spika wa bunge la Afrika Mashariki Abdurahman Kinana anayetokea nchini Tanzania. Itakumbukwa kwamba katika uchaguzi wa mwaka 2007 katika taifa hilo la Afrika Mashariki baadhi ya viongozi wa kisiasa walivitupia lawama vyombo vya waangalizi wa kigeni kwa kudai vinatoa ripoti ambazo hazina ukweli vilipodai  kwamba kulikuwepo udanganyifu katika uchaguzi huo ambao matokeo yake yalitangazwa kwa njia za utata ghafla na aliyekuwa wakati huo mkuu wa tume ya uchaguzi Samuel Kivuitu baada ya kuzuka vurugu katika ukumbi yalikokuwa yakitangazwa matokeo ya mwisho ya uchaguzi huo.

Tume ya waangalizi ya Umoja wa Ulaya ilisema uchaguzi huo wa mwaka 2007 ulikosa kuzingatia sheria muhimu za Kimataifa na zile za kikanda za uchaguzi wa kidemokrasia, kwa mujibu wa tume hiyo utaratibu mzima wa kuhesabu na kutangaza matokeo ulikumbwa na hali ya kukosekana uwazi  jambo ambalo lilisababisha kucheleweshwa kwa matokeo ya urais na hatimaye wananchi wakapoteza subira  hali iliyozusha vurugu zilizogeuka kuwa vita kamili vya kikabila.

Je waangalizi wa uchaguzi kutoka nje watakuwa na mchango gani na wamejiandaa vipi katika kuepusha lawama.Katika Kinaga Ubaga Saumu Mwasimba amezungumza na kiongozi wa kundi la waangalizi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki AbdulRahman Kinana na kwanza anataka kujua maandalizi yeo yamefikia wapi katika kuusimamia uchaguzi wa Kenya Marchi nne.

Kusikiliza mahojiano hayo bonyeza alama ya kusikiliza masikioni hapo nchini

Mwandishi: Saumu Mwasimba
Mhariri:Josephat Charo