1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waangalizi wa jumuiya ya madola wasema uchaguzi wa Rwanda shwari

Josephat Nyiro Charo11 Agosti 2010

Rais Paul Kagame ameshinda awamu ya pili ya miaka saba dhidi ya wapinzani wake watatu waliomuunga mkono katika uchaguzi wa mwaka 2003

https://p.dw.com/p/OifO
Rais wa Rwanda, Paul KagamePicha: DW

Rais wa Rwanda Paul Kagame ataiongoza nchi hiyo kwa awamu nyingine ya miaka saba baada ya kushinda uchaguzi wa rais uliofanyika siku ya Jumatatu wiki hii nchini humo. Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamemkosoa kiongozi huyo kwa kuukandamiza uhuru wa upinzani na uhuru wa vyombo wa vyombo vya habari wakati wa kampeni yake. Mwandishi wetu wa mjini Kigali,

Daniel Gakuba, alizungumza na Dr Salim Ahmed Salim, aliyeuongoza ujumbe wa waangalizi wa jumuiya ya madola katika uchaguzi huo wa Rwanda, kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi nchini humo. Akizungumzia kwanza uhuru wa vyombo vya habari Dr Salim alikuwa na haya ya kusema.

Insert Interview: Dr Salim - Daniel Gakuba

Mhariri: Josephat Charo