1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waangalizi waridhika na maandalizi ya uchaguzi

3 Machi 2013

Huku ikiwa zimesalia chini ya saa 24 kabla ya zoezi la uchaguzi mkuu kuanza nchini Kenya, makundi ya waangalizi nchini humo yameonyesha kuridhika na jinsi maandalizi ya uchaguzi huo yanavyoendelea.

https://p.dw.com/p/17pNT
epa03307523 Nkosazana Dlamini-Zuma of South Africa leaves the room after giving a press conference during the 19th African Union Summit in Addis Ababa, Ethiopia, 15 July 2012. South Africa's home affairs minister Nkosazana Dlamini-Zuma is challenging incumbent Jean Ping of Gabon for the bloc's top job after both of them failed to win the required two-thirds majority of the vote at the last summit. If the election fails again this time, it could leave Ping in position until the next summit in January 2013. EPA/MARTIN DIXON +++(c) dpa - Bildfunk+++
Rais wa halmashauri kuu ya umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini-ZumaPicha: picture-alliance/dpa

Katika kikao na waandishi wa habari, rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Mataifa ya Afrika, AU, Bi Nkosazana Dlamini Zuma amesema kuwa ujumbe wake umekutana na Rais Mwai Kibaki na kuwahakikishia kuwa shughuli za uchaguzi zitafanywa kwa njia ya amani.

Aidha kiongozi huyo alikutana pia na viongozi wa vyama mbalimbali, maafisa wa Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka na pia Inspekta Mkuu wa Jeshi la Polisi ambao wote walimwelezea kuridhika kwao na matayarisho ya uchaguzi.

A woman walks past a message of peace in Kibera slum in the capital Nairobi February 28, 2013. Kenya will hold its general elections on March 4. REUTERS/Noor Khamis (KENYA - Tags: ELECTIONS POLITICS)
Ujumbe wa kuhimiza amani eneo la Kibera, NairobiPicha: Reuters

"Wakenya wako tayari kwenda kwenye uchaguzi mnamo Jumatatu na ujumbe wetu umekutana na baadhi ya wagombea wa kiti cha Urais na wako tayari kupiga kura kwa amani na kukubali matokeo".

Bi Zuma aliandamana na aliyekuwa Rais wa zamani wa Msumbiji Joachim Chissano, ambaye ni kiongozi wa waangalizi wa Umoja wa Mataifa ya Afrika. Alisema kulikuweko na hali ya taharuki katika maeneo kadha nchini kufuatia uvumi kuwa baadhi ya watu walikuwa wanasambaza vikaratasi kwa nia ya kueneza chuki, japo walipewa hakikisho kuwa suala hili lilikwisha dhibitiwa na polisi. Chisano anahimiza wagombea wazingatie imani walionayo kwa katiba na kuwasilisha malalamiko yote kortini.

"Bi Dlamini ametoa mwito kwa Wakenya kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya Jumatatu ili kumchagua kiongozi wampendaye.

Wakati huo huo amewahimiza wale wanaowania viti vya uongozi waitikie uamuzi wa wananchi".

"Washindi waitikie ushindi kwa unyenyekevu na kwa wale watakao shindwa wakumbuke kwamba bado wanahitajika katika ujenzi wa taifa.Tunatumai mambo yatakuwa shwari".

Zaidi ya waangalizi wapatao 20,000 kutoka makundi mbali mbali, miongoni mwao wale kutoka Jumuiya ya Ulaya, Umoja wa Kiafrika na Jumuiya ya Afrika Mashariki wamo nchini Kenya kwa shughuli ya hii muhimu.

Mwandishi: Reuben Kyama / DW correspondent/ Nairobi

Mhariri : Sekione Kitojo