1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa Chad wataka mazungumzo na serikali

21 Juni 2008

-

https://p.dw.com/p/ENox

NDJAMENA

Waasi nchini Chad wamebadilisha ghafla mtizamo wao na kutoa mwito wa kutaka mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo ikiwa ni siku chache baada ya kutokea mapambano makali kati yao na wanajeshi wa serikali.

Msemaji wa waasi Ali Gueddei hapo jana alisema kundi lake liko tayari kukaa chini na serikali kujadiliana juu ya matatizo yanayowakabili wananchi wa Chad kwa lengo la kutafuta suluhisho la kudumu katika mgogoro wa nchi hiyo. Mapema wiki hii waasi hao walipambana na wanajeshi wa serikali katika eneo la Am Zoer kilomita 80 kutoka kaskazini mwa mji wa Abeche ambapo walidai ushindi na kutishia kuongeza nguvu mapambano hayo kuelekea mji mkuu Ndjamena.