1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa Darfur wakubali uchunguzi ufanywe katika miji mitatu

11 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D5tE

Waasi wa Darfur wamesema wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika wanaweza kuchunguza mashambulio yanayofanywa na serikali ya Sudan katika miji mitatu ya Darfur Magharibi.

Hata hivyo waasi hao wameonya dhidi ya kupeleka kikosi cha kimataifa katika eneo hilo.

Serikali ya Sudan katika uvamizi wake mkubwa katika kipindi cha miezi kadhaa, Ijumaa iliyopita iliishambulia miji ya Abu Surouj, Sirba na Suleia na kuwalazimisha raia takriban 200,000 kuyakimbia makazi yao.

Kiongozi wa kundi la waasi linalopigania haki na usawa, JEM, Khalil Ibrahim, amesema wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika wanakaribishwa kufanya uchunguzi katika eneo hilo lakini hawapaswi kukaa.

Hapo awali kiongozi huyo ameonya kwamba wanajeshi wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa watakaopelekwa katika eneo hilo wanakabiliwa na hatari ya kushambuliwa.