1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa FDLR sasa wajificha

23 Agosti 2012

Kundi la wanamgambo wa Kihutu kutoka Rwanda la FDLR linaonekana hadi sasa kuwa kundi la waasi linalojihusisha na matendo ya kinyama kabisa katika eneo la mashariki ya Congo .

https://p.dw.com/p/15vKj
A government soldier looks on as a man carries a boy with a bullet wound in his leg in the eastern Congolese town of Rumangabo, July 26, 2012. Congolese M23 rebels and government forces traded heavy weapons fire around two eastern villages on Thursday in another round of fighting that has forced thousands of civilians to flee towards the provincial capital Goma. REUTERS/James Akena (DEMOCRATIC REPUBLIC OF CONGO - Tags: CIVIL UNREST POLITICS CONFLICT)
Wakimbizi mashariki ya KongoPicha: Reuters

Kwa muda wa miaka 16 sasa kundi hilo limekuwa likiwatia hofu,kupora na kuharibu mali pamoja na kuwauwa kwa makusudi raia wa eneo hilo. Katika misitu ya eneo hilo wameunda taifa ndani ya taifa , ikiwa ni serikali iliyoko uhamishoni pamoja na jeshi ambalo halisiti kutumia ukatili wakati wote. Lengo lao ni kuirejesha Rwanda mikononi mwao na serikali inayoongozwa na Watutsi ya rais Paul Kagame waiondoe madarakani.

Kundi la wanamgambo wa FDLR , ikiwa na maana ya jeshi la ukombozi wa Rwanda linatoa sababu zinazozusha vita kadha na mizozo kati ya nchi jirani ya Rwanda na jamhuri ya kidemokrasi ya Congo. Kwanza katika mwaka 2009 serikali zote mbili zilikubaliana , kufanya operesheni ya pamoja , ili kuweza kuwasaka waasi wa kundi la FDLR. Kutokana na kuzuka kwa kundi hivi karibuni la waasi wa M23 , operesheni hii ya kijeshi ilibidi kusitishwa.

Kwa hiyo kundi la FDLR hivi sasa linajikuta katika hali ya mchanganyiko. Makamanda wake wanakimbia.

Ignace M. während eines Interviews am 14.10.2008 in dem MDR-Beitrag "Kriegsverbrecher" der TV-Sendung "Fakt" am 03.11.2008. Grausame Massaker der Hutu-Miliz FDLR im Ost-Kongo sollen von Deutschland aus gelenkt worden sein. Die Bundesanwaltschaft ließ am Dienstag (17.11.2009) den in Mannheim lebenden und von Ruanda als Kriegsverbrecher gesuchten Ignace M. in Karlsruhe verhaften. Foto: MDR/Fakt (bestmögliche Qualität) - zu dpa 4454 vom 17.11. +++(c) dpa - Bildfunk+++
Rais wa kundi la FDLR Ignace MurwanashyakaPicha: picture-alliance/dpa

Himaya ya FDLR

Kilometa chache upande wa kaskazini ya eneo la mashariki ya Congo inaanza ile inayojulikana kama mamlaka ya waasi wa Kihutu wa FDLR. Mnaweza kuingia katika eneo letu, wanajeshi wetu wanahabari ya ujio wenu, ameandika waziri wa habari wa FDLR Laforge Fils Bazaye katika taarifa. Amemwalika mwandishi wa habari hii kwa mahojiano.

Kandokando ya barabara tayari wamejipanga wapiganaji wa FDLR. Wanamgambo hao wa Kihutu wanaonekana kuwa ni kundi linalotumia mbinu za kinyama kabisa katika mashariki ya Kongo. Kundi hili liliundwa katika kambi ya wakimbizi , na baada ya hapo wale waliohusika na mauaji ya kimbari mwaka 1994 nchini Rwanda walikimbilia mashariki ya Congo. Pia katika duru za uongozi wa FDLR wamo wahusika kadha wa mauaji hayo ya kimbari. Miaka 16 hadi sasa FDLR wanadhibiti eneo , ambalo ni kubwa kuliko nchi yao ya Rwanda. Katika wakati ambao walikuwa na nguvu kubwa walikuwa na wapiganaji zaidi ya 20,000.

Waziri wa habari wa FDLR Laforge Fils Bazaye anafafanua lengo la kundi hili.

"Malengo ya kundi letu ni kama ifuatavyo: Kwanza , ni kuwalinda wakimbizi, ambao wamo katika awamu ya mwisho ya kumalizwa kabisa na jeshi la Rwanda, kwa ruhusa rasmi ya serikali ya Congo. Pili; Ni kuikomboa Rwanda chini ya utawala wa dikteta mhalifu Paul Kagame. Tangu ilipoundwa FDLR tunapambana. Kwasababu tangu kuharibiwa kwa kambi za wakimbizi mashariki ya Congo , jeshi hilo halijawaacha wakimbizi katika hali ya amani hata mara moja. Wakimbizi wamekuwa kila mara wakiwindwa, na hilo ni mpaka hivi leo".

Families fleeing renewed fighting between the government and M23 rebels near Kibumba walk toward the eastern Congolese city of Goma July 25, 2012. Congolese rebels and government forces traded heavy weapons fire around two eastern villages on Friday, forcing thousands of civilians to flee towards the provincial capital days ahead of a regional summit due to tackle the rebellion. REUTERS/James Akena (DEMOCRATIC REPUBLIC CONGO - Tags: CIVIL UNREST POLITICS CONFLICT TPX IMAGES OF THE DAY)
Wakimbizi wakijisalimisha na mapiganoPicha: Reuters

Rais wa FDLR kizimbani

Rais wa FDLR Ignace Murwanashyaka na makamu wake Straton Musoni wanaishi kama wakimbizi nchini Ujerumani wakiwa na hadhi ya wakimbizi wa kisiasa. Kwa kupitia simu na barua pepe wanaongoza mapambano ya kundi lao. Lakini katika mwaka 2009 viongozi wote hao wawili wa FDLR walikamatwa na mwaka 2011 walifikishwa mbele ya sheria. Hali hii imekuwa ni pigo kubwa kwa FDLR na imesababisha kudhoofika kwa kiasi kikubwa, hususan katika morali wa mapambano. Lakini msemaji wa FDLR Bazaye anapinga hilo.

"Ni kutokana na sababu za kisiasa ndio alikamatwa , ndio sababu hakuweza moja kwa moja kuhukumiwa. Watu wanahisi kuwa iwapo rais na makamu wake wamekamatwa, ni sawa na kukata kichwa cha FDLR, na hapo watu wengine wanavunjika moyo na kusalim amri. Lakini hali hiyo haikutokea. Hatumfuati mtu mmoja , badala yake tunafuata nadharia. Ignace Murwanashyaka anaweza kukamatwa pamoja na makamu wake, lakini mapambano yetu yanaendelea".

A government soldier holds a position in the eastern Congolese town of Rumangabo, July 26, 2012. Congolese M23 rebels and government forces traded heavy weapons fire around two eastern villages on Thursday in another round of fighting that has forced thousands of civilians to flee towards the provincial capital Goma. REUTERS/James Akena (DEMOCRATIC REPUBLIC OF CONGO - Tags: CIVIL UNREST POLITICS CONFLICT)
Wapiganaji waasi wakipambana mashariki ya CongoPicha: Reuters

Waziri wa habari wa FDLR Laforge yuko pamoja na makamanda watatu katika chumba cha ofisi yake na anakunywa bia katika glasi kubwa. Kuzunguka jengo hilo la mbao kuna wapiganaji waliobeba bunduki za Kalashnikov. Anaishi siku hizi mwendo wa miguu wa siku tatu kaskazini magharibi ya Kalembe , anaeleza katika kijiji cha Maniema. Huko wamewaweka makamanda wa ngazi ya juu na wake zao na watoto katika maeneo ya usalama, ikiwa ni jumla ya watu elfu kadha , anasema waziri huyo wa habari.

"Tangu mwaka 1996 wakimbizi wamekuwa wakiuwawa , hadi hii leo. Tangu pale jeshi la Rwanda lilipoamua kuwa linataka kuwabana wapiganaji wa FDLR na kuwafyeka wakimbizi wote, mkakati sasa umebadilika. Sasa wamewachukua wapiganaji wa Congo, na wanawapatia fedha, na serikali ya Congo inawapa silaha. Wanawapa fedha wanamgambo hawa wa Congo, ili wapigane na sisi pamoja na wakimbizi wote wa Kihutu kutoka Rwanda katika eneo hili la mashariki ya Congo, wakiwa watoto , wanawake ama wazee. Hili ndio tatizo letu tangu mwishoni mwa mwaka 2011".

Wapiganaji wanasakwa

Kwa miezi kadha sasa viongozi wa wanamgambo hao wa FDLR wako mafichoni.Hali katika eneo la mashariki ya Congo imebadilika na kuwa mbaya sana. Mwezi Aprili walikimbia maafisa kadha na wapiganaji wao kutoka katika maeneo ya wanajeshi wa Congo. Wengi wao walikuwa maafisa wa zamani wa waasi wa wanamgambo wa CNDP, ambao katika mwaka 2009 waliingizwa katika jeshi la Congo. Tangu wakati huo jeshi la Congo linajikuta katika mapambano dhidi ya kundi hili jipya la waasi, ambalo linajiita M23. Jeshi la Congo limechukua hatua ya kupambana dhidi ya FDLR. Uchunguzi wa umoja wa mataifa umebaini kuwa kundi la M23 linapata usaidizi kutoka Rwanda. Hali hii imesababisha mataifa kadha washirika ya Ulaya pamoja na Marekani kuchukua hatua, ya kupunguza fedha za misaada ama kusitisha kabisa, ambapo mbinyo huu wa kisiasa dhidi ya hasimu mkubwa Rwanda imekaribishwa na kundi la FDLR, anasema Bazaye.

Mwandishi: Schlindwein, Simone / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri : Mohammed Abdul Rahman.