1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wasamabaratisha vikosi vya Gaddafi

29 Machi 2011

Taarifa kutoka Libya zinasema waasi wamevisambaaratisha Vikosi vinavyomuunga mkono,Kiongozi wa Libya Muammer Gaddafi pamoja na vifaru.

https://p.dw.com/p/10joC
Waasi nchini Libya
Waasi nchini LibyaPicha: dapd

Taarifa za sasa zinasema zaidi ya watu 142 wamepoteza maisha na wengine zadi ya 1400 kujieruhiwa wakiwemo wengine 90 wakiwa katika hali mbaya.

Hivi sasa vikosi vya wanajeshi wanaomtii kanali Gaddafi vimeweka kambi katika eneo moja mjini Misrata lililopo mashariki mwa mji wa Tripoli.

Akizungumza kwa masharti ya kutotajwa jila lake muasi mmoja anasema, vikosi hivyo kwa hivi sasa vinajiandaa kufanya mashambulizi dhidi yao.

Amedai hivi sasa Misrata ipo katika tishio la kutokea mauwaji ya haraiki na kuongeza kwamba kile kilichozuiwa Benghazi na vikosi vya muungao kitarajiwe kutokea eneo hilo.

Mtu mwingine ambae ni daktari,amesema katika mapigano yaliyotokea leo mjini Misrata watu wanne wamepoteza maisha.

Waasi wa Libya wakishangilia
Waasi wa Libya wakishangiliaPicha: AP

Kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya majeruhi hivi sasa kuna matarajio kwa meli Kituruki kwenda kuchukua majeruhi takribani 50 katika eneo hilo kwa matibabu zaidi.

Awali msemaji wa Waasi,Shamsidin Abdulmolah amesema meli hiyo,ambayo ina hospitali ndani yake, inayosindikizwa na vikosi vya NATO itachelwa kuwasili mjini Misrata.

Kuwasili kwa meli hii kulitanguliwa na meli nyingine kubwa iliyobeba misaada ya vyakula, maziwa na vitu vingine muhimu kwa binadamu.

Katika hatua nyingine, serikali ya Libya leo iliwapeleka Waandishi wa habari kwenda kujionea mambo yalivyo katika eneo hilo,tukio ambalo lilioneshwa moja kwa moja na televisheni ya taifa ya nchi hiyo.

Hata hivyo, baadhi ya Waandishi, wamesema hawakupelekwa eneo la kati la mji ambako kulionekana dhahiri mapigano yanaendelea kutokana na kutanda kwa moshi mzito.

Waasi wanadai vikosi vinavyomtii,Gaddafi vimesababisha kaya zaidi ya elfu tano bila ya makazi na kuongeza kuwa hivi sasa vinashikilia eneo la kaskazini la Misrata.

Kauli zinapishana katia ya Waasi na Serikali ya Libya ambapo serikali inasema vikosi vyake vimesimamisha mashambulizi mjini humo na kwamba hivi mji upo mikononi mwao na umekuwa shwari kabisa.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Shirika la Habari la Libya, inadai kikosi cha kupambana na ugaidi kimesitisha mashambulizi dhidi ya raia yaliyokuwa yakifanywa na magaidi.

Katika tukio lingine televishen ya Taifa ya Libya, iliyokuwa ikitangaza moja kwa moja katia makazi ya Gaddafi mjini Tripoli mapema,imemuonesha mtoto wa kiongozi huyo Hamis ambae ilitangazwa kuwa amefariki baada ya kujeruhiwa na makombora ya majeshi ya Muungano.

Majeshi ya Muungano yalianza operesheni za kuzuia ndege kuruka nchini Libya machi 19 kwa shabaha ya kuwanusuri wananchi na mashambulizi ya serikali ya nchi hiyo ambayo hata hivyo yametoa fursa kwa Waasi kusonga mbele.

Mwandishi:Sudi Mnette /rtr,afp

Mhariri: Abdul-Rahman