1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
BiasharaMarekani

Wabunge Marekani wahoji uhusiano wa Afrika Kusini na Urusi

15 Juni 2023

Kundi la wabunge nchini Marekani wametaka mkutano muhimu wa kibiashara kati ya Marekani na Afrika uliopangwa kufanyika nchini Afrika Kusini baadae mwaka huu, kuhamishwa kutokana na uhusiano unaongozeka na Urusi.

https://p.dw.com/p/4SarP
Mkutano wa BRICS nchini Brazil /Vladimir Putin na Cyril Ramaphosa
Marais wa Afrika Kusini na UrusiPicha: Mikhail Metzel/ITAR-TASS/IMAGO

Afrika Kusini inatazamiwa kuwa mwenyeji wa Kongamano la AGOA mjini Johannesburg,ambao ni mkutano wa viongozi wa Afrika na maafisa wa Marekani kujadili mustakabali wa mpango huo, ambao unatarajiwa kuisha mwaka 2025.

Katika barua ilioolekezwa kwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken na wakuu wengine,wabunge hao wasioegemea upande wowote pia walipendekeza kwamba Afrika Kusini ipo kwenye hatari ya kupoteza manufaa yake chini ya Sheria ya Ukuaji na Fursa ya Afrika AGOA, ambao ni mpango mkuu wa biashara wa Washington.

Afrika Kusini mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa BRICS
Mawaziri wa mambo ya nje wa jumuiya ya BRICSPicha: Foreign Ministry Press Service/ITAR-TASS/IMAGO

Sehemu ya barua hiyo ilioandikwa mnamo June 9 ilionesha wasiwasi juu ya mwenyeji wa mkutano na hapa nina nukuu "tuna wasiwasi mkubwa kwamba kuandaa Kongamano la AGOA la 2023 nchini Afrika Kusini kutakuwa kama uidhinishaji wa wazi wa uungwaji mkono wa Afrika Kusini kwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Akirejelea barua hiyo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Afrika Kusini Clayson Monyela aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter kwamba hakuna uamuzi wa Wizara ya Mambo ya Nje wala Ikulu ya Marekani kuhamisha kongamano hilo la AGOAkutoka Afrika Kusini.

Idara ya Biashara na Viwanda ya Afrika Kusini, ambayo inasimamia uhusiano wa kibiashara wa nchi hiyo na Marekani, imesema haikupanga kujibu barua hiyo hadharani.Kufuatia pingamizi hilo la kundi la wabunge nilimuuliza mchambuzi wa masuala ya diplomasia na uchumi kutoka Johanesburg ... hatua inaathiri vipi mahusiano ya pande hizo?

Soma kuhusu: Mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la BRICS wakutana Afrika Kusini

Ikumbukwe kwamba mauzo ya Afrika Kusini kwenda Marekani chini ya mpango wa AGOA yalifikia karibu dola bilioni 1 katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu, na kuifanya kuwa mnufaika wa pili wa mpango huo baada ya Nigeria.

Mataifa ya Afrika yanatafuta kuongeza muda wa AGOA, ambayo inatoa ruzuku ufikiaji wa upendeleo wa mauzo ya nje wa nchi zinazofaa kwa Marekani.Lakini kuongezeka kwa mafungamano ya kijeshi kati ya taifa hilo na Urusi limeendelea kutia shubiri mahusiano yake na mataifa ya Magharibi.

BRICS mkutano kwa njia ya video 2021
Viongozi wa Jumuiya ya BRCSPicha: BRICS Press Information Bureau/AP/picture alliance

Serikali ya Afrika Kusini ilitangaza kutoegemea upande wowote katika vita vya Ukraine, na Rais Cyril Ramaphosa anashiriki katika juhudi za viongozi wa Afrika kupatanisha mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Hata hivyo, wabunge hao walionyesha kusikitishwa na jinsi Afrika Kusini ilivyoandaa oparesheni za pamoja za jeshi la majini kati ya China na Urusi mwezi Februari, na wanapanga kufanya mkutano wa kilele wa viongozi wa BRICSambapo Rais wa Urusi Vladimir Putin amealikwa licha ya kushtakiwa kwa uhalifu wa kivita na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu.

Wabunge hao pia waliunga mkono shutuma za  Balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini, kwa taifa hilo kuidhinisha meli ya Urusi kukusanya na kuhamisha silaha katika kambi ya wanajeshi wa majini mwaka jana. Maafisa wa Afrika Kusini wanasema hawajui kuhusu uhamisho huo wa silaha na wameanzisha uchunguzi huru kuhusu uhamishaji huo.