1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wabunge wapitisha mswada wa mageuzi ya afya nchini Marekani.

Halima Nyanza22 Machi 2010

Hatimaye, baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa majadiliano makali yaliyojaa mabishano, Baraza la Wawakilishi nchini Marekani limepitisha mswada wa mageuzi ya huduma ya afya nchini humo.

https://p.dw.com/p/MYxt
Rais Barack Obama wa marekani akizungumza baada ya Baraza la wawakilishi nchini humo kupitisha muswada wa mageuzi ya ya mfumo wa afya nchini humo.Picha: AP

Mswada wapitishwa: Baraza la Wawakilishi nchini Marekani limepitisha mswada huo kwa kura 219 kwa 212, huku wabunge wote 178 kutoka chama cha Republican na 34 kutoka chama cha Democrat waliupinga mswada huo, wenye lengo la kuwapatia bima ya afya Wamarekani wapatao miloni 32, ambao hivi sasa hawana kinga yoyote na mradi huo unakadiriwa kugharimu dola 940 katika kipindi cha miaka 10.

Mehrheit für Gesundheitsreform in den USA Flash-Galerie
Baraza la wawakilishi nchini Marakani likipigia kura mswada wa mabadiliko ya mfumo wa afya nchini humo.Picha: AP

Obama afurahishwa: Akizungumza mara tu baada ya baraza la wawakilishi kuupigia kura mswada huo, akiwa ameongozana na Makamu wa Rais wa nchi hiyo Joe Biden, Rais wa Marekani, Barack Obama amelisifu baraza hilo kwa kuweza kuupigia kura mpango wake huo na kusema kuwa ni ushindi kwa Wamarekani na kwamba haikuwa rahisi kwa watu wengi, lakini ilikuwa ni jambo sahihi na kwamba ameielezea kura hiyo kama majibu ya sala ya kila Mmarekani ambaye alikuwa na matumaini ya kufanyika kwa kitu fulani kuhusu mfumo wa huduma ya afya ambao unafanyakazi kwa makampuni ya bima na si kwa watu wa kawaida.

Aidha Rais Obama ambaye alikuwa akilifuatilia zoezi hilo la upigaji kura akiwa katika Ikulu ya nchi hiyo pamoja na wasaidizi wake, amesema kupitishwa kwa muswada huo sio tu kutawasaidia watu ambao hawana bima ya afya, lakini pia utasaidia wale wole walio na bima na kwamba kuidhinishwa kwa muswada huo kunathibitisha kwamba serikali ni ya watu wote na kwamba inaendelea kuwatumikia watu wake.

Ameongezea kusema kuwa suala la mageuzi ya afya nchini humo, halikuwa jambo rahisi kwa watu wengi, lakini ilikuwa ni jambo sahihi hususan kwa raia wa nchi hiyo na kwamba ni ushindi wa watu wa Marekani.

Aidha matokeo hayo ya kura yameelezwa kuwa ni ushindi mkubwa kwa rais Obama ambaye katika kampeni zake za kuwania kiti cha Urais suala la mageuzi katika sekta ya afya alilipa kipaumbele, na kwamba mswada huo ni wa kihistoria nchini humo kwa kipindi cha miaka kadhaa iliyopita.

Ili kuweza kufanikisha kupitishwa kwa muswada huo, baraza la wawakilishi pia lilifanyia marekebisho vipengele kadhaa ya mswada huo.

Maandamano kuupinga: Wakati baraza la wawakilishi lilipokuwa likikutana kuupigia kura mswada huo waandamanaji kadhaa walikusanyika nje ya majengo ya bunge kupinga muswada huo.

Proetste gegen Gesundheitsreform in Washington
Waandamanani waliokusanyika nje ya baraza la wawakilishi kuupinga mpango huo.Picha: picture alliance/dpa

Mwandishi: Halima Nyanza(dpa,Reuters,afp)

Mhariri: Josephat Charo