1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafanyakazi wahamiaji wahofia ubaguzi Ujerumani

John Juma
30 Januari 2024

Ujerumani inahitaji wafanyakazi wenye taaluma mbalimbali kutoka nchi za nje na waziri wake wa kazi na ajira amesaini mpango na Vietnam. Lakini wahamiaji wanahofia ubaguzi wa rangi unaoongezeka nchini Ujerumani.

https://p.dw.com/p/4bos4
Vietnam | Waziri wa Ajira Ujerumani Hubertus Heil na mwenzake wa Vietnam Dao Ngoc Dung
Waziri wa Ajira Ujerumani Hubertus Heil baada ya kusaini hati ya makubaliano ya masuala ya ajira na waziri wa ajira Vietnam Dao Ngoc Dung.Picha: Bernd von Jutrczenka/dpa/picture alliance

Wakati rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier na waziri wa kazi na ajira Hubertus Heil walipowasili katika chuo kikuu cha ushirikiano wa Vietnam na Ujerumani (VGU) mjini Ho Chi Minh, walipigwa na mshangao kuwaona wanafunzi waliowashangilia na kuwasalimu kwa bashasha.

Baadhi ya wanafunzi hao wataelekea Ujerumani kufanya kazi katika kampuni za taifa hilo lenye Uchumi mkubwa zaidi katika Umoja wa Ulaya.

Hali ilikuwa kama hiyo wakati ujumbe huo wa Ujerumaniulipowasili katika taasisi ya Goethe mjini Hanoi, ambapo kila mwaka takriban vijana 6,000 wa Vietnam husomea lugha ya Kijerumani.

Idadi hiyo mara saba ya vijana nchini humo, hujisajili kusomea lugha hiyo kuwawezesha kupata mafunzo ya kitaaluma au masomo zaidi nchini Ujerumani.

Soma pia:Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz azitolea mwito nchi wanachama wa EU waongeze msaada wa fedha kwa Ukraine

Mwishoni mwa mwaka 2023, Ujerumani ilianza kutekeleza sheria yake mpya ya uhamiaji unaolenga wataalam, kwa kutumia mfumo unaozingatia alama ili kupunguza vikwazo vinavyowakabili wafanyakazi wenye ujuzi na wanataka kuhamia Ujerumani.

Tangu wakati huo, wanasiasa wa ngazi za juu wa Ujerumani wamekuwa wakiongeza juhudi za kuwashawishi wafanyakazi wenye ujuzi katika nchi nyingine.

Hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Nje Annalena Baerbock alikuwa Ufilipino huku waziri wa Misaada ya Maendeleo Svenja Schulze alizuru Morocco.

Huko Vietnam, Steinmeier na Heil walitia saini mkataba wa makubaliano ambao unaboresha utaratibu wa uhamiaji wa wafanyikazi kwenda Ujerumani.

Wavietnam wanaziona fursa za kazi Ujerumani

Kuna idadi kubwa ya Wavietnam ambao wanataka kufanya kazi Ujerumani. Inakadiriwa kuwa kuna tayari Watu 200,000 kutoka Vietnam wanaoishi nchini Ujerumani, taifa ambalo ni la kikomunisti. 

Berlin, Ujerumani | Wafanyakazi wa sekta ya afya
Wafanyakazi wa sekta ya afya ya UjerumaniPicha: Political-Moments/IMAGO

Phuong Phan, mwenye umri wa miaka 22 anatarajia atafanya kazi katika sekta ya hoteli katika jimbo la Thuringia, Ujerumani mashariki. Jimbo hilo ndilo la kwanza kusaini mikataba za pande mbilina Vietnam.

Soma pia:Bunge la Ujerumani lapiga kura kurahisisha sheria ya kupata uraia pacha

Hata hivyo, hivi karibuni, Phuong Phan, alipata jambo ambalo halikumpendeza sana. Ripoti zinazoelezea chuki dhidi ya wageni ambayo wakati mwingine hushuhudiwa nchini Ujerumani, haswa mashariki.

Hataki kulizungumzia katika mazungumzo yake na DW lakini anasema mada hiyo pia imeshughulikiwa katika kozi zake za lugha.

Nguyen Thi Thanh Tam, afisa anayehusika na usajili huko Thuringia, amekiri kuwa wameanza kuwa na mashaka kuhusu hofu hizo.

Kampeni ya kutafuta wafanyakazi Ujerumani

Kulingana na Shirika la Shirikisho la Ajira la Ujerumani (BA), nchi hiyo ina nafasi za kazi milioni 1.73 zilizoachwa wazi.    

Tofauti na kampeni ya Ujerumani ya kutafuta wafanyikazi miaka 60 iliyopita, juhudi za sasa hazilengi vibarua viwandani bali wataalamu waliohitimu sana na watu walio na uzoefu katika sekta ya huduma.

Wakati huo, watu chini ya 300,000 pekee walikuja kila mwaka. Kwa sasa, tafiti zinasema Ujerumani inahitaji karibu 400,000 kwa mwaka.

Ujerumani: Rasimu ya kuwarudisha watu katika mataifa yao

Kwa kuzingatia mageuzi mazuri ya uhamiaji wa wafanyikazi, ripoti za hivi karibuni kuhusu makundi yanayochochea ubaguzi wa rangi nchini Ujerumani zinawatia baadhi wasiwasi zaidi.

Soma pia:Ujerumani huenda ikawatimua maelfu ya waomba hifadhi wa Nigeria

Waziri wa Kazi Heil aliliambia shirika hili la habari la DW kwamba hakuna mtu aliyezungumza naye moja kwa moja kuhusu suala hilo lakini hatua inahitaji kuchukuliwa kabla maji kuzidi unga.

Hivi karibuni kulishuhudiwa maandamano makubwa dhidi ya chama mbadala kwa UjerumaniAFD ambacho kinawapinga wageni.

Wavietnam wanaoishi Ujerumani pia wana wasiwasi. Mmoja wao ni Huong Trute, ambaye Rais Steinmeier alimwalika kuandamana naye katika safari yake ya Vietnam.