1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafugaji Dodoma wadai haki zao

20 Aprili 2017

Ni malalamiko ya wafugaji mjini Dodoma juu ya kile wanachodai ni manyanyaso kutoka Manispaa kukamata mifugo yao mara kwa mara na kutozwa faini. Maeneo ya malisho kwa mifugon yamepungua baada ya mji kupanuka.

https://p.dw.com/p/2ba2v
Wafugaji na mifugo ya Dodoma
Picha: DW/A. Mtalika

RIPOTI WAFUGAJI MANISPAA YA DODOMA - MP3-Stereo

Mkoa wa Dodoma kiasili ni wa wakulima na wafugaji kwani ndio shughuli za asili za kutafuta kipato cha kuendesha maiasha ya kila siku kwa familia mbalimbali.

Wafugaji wakiwa wamekusanyika nje ya ofisi za Manispaa ya Dodoma kutaka kujua hatima ya ya mifugo yao iliyokuwa imekamatwa
Wafugaji wakiwa wamekusanyika nje ya ofisi za Manispaa ya Dodoma kutaka kujua hatima ya ya mifugo yao iliyokuwa imekamatwaPicha: DW/A. Mtalika

Kutokana na asili hiyo basi baadhi ya wananchi wamekuwa na wakiendelea na utamaduni wa kufuga pamoja na miji kuendelea kukua na kuwa si rafiki kwa shughuli za ufugaji wa asili kwa maana ya kutoa mifugo na kupeleka maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuipatia malisho kwa maana majani yaani machungani.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunamabi akitoa maelekezo kwa wafugaji
Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunamabi akitoa maelekezo kwa wafugajiPicha: DW/A. Mtalika

DW imezungumza na baadhi ya wafugaji hao ambao wanaonekana kuchukizwa na kitendo cha kukamatwa mifugo wakisema ikiwezekana watengewe maeneo ya kufugia. Mbali na kukamatwa mifugo, lakini pia wanalalmikia juu ya kutozwa faini bila kupewa risti, jambo ambalo anasema huenda ni utapeli