1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafungwa wa Kipalestina waachwa huru.

3 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CW3n

Jerusalem. Israel itawaacha huru wafungwa 429 Wapalestina leo Jumatatu. Wafungwa wa kwanza tayari wamekwisha pelekwa katika kituo cha upekuzi nje ya mji wa Ramallah ulioko katika ukingo wa magharibi , ambako kutoka huko wataingia katika mamlaka ya Palestina. Walioachiliwa huru ni wanachama wa kundi la Fatah linaloongozwa na rais Mahmoud Abbas. Wapiganaji wa kundi lenye imani kali ya Kiislamu Hamas hawataachiwa.

Wakati huo huo chama cha Hamas kimesema kuwa mpiganaji wake mmoja ameuwawa na wengine watano wamejeruhiwa kwa makombora ya Israel , saa chache baada ya wapiganaji hao kufyatua kombora dhidi ya eneo la Israel. Jeshi la Israel limethibitisha kuwa limeshambulia kwa makombora wapiganaji hao katika eneo nje ya mji wa Gaza, kufuatia shambulio la kombora kutoka kwa Wapalestina ambalo limewajeruhi wanajeshi watatu wa Israel.