1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waganda waigomea kampuni ya China kwa unyanyasaji kingono

Sekione Kitojo
5 Januari 2017

Wafanyakazi 400 wa Uganda wameanza mgomo wakilalamikia unyanyasaji wa kingono unaofanywa na mameneja wa kampuni ya Kichina wanayoifanyia kazi mjini Kampala.

https://p.dw.com/p/2VEca
Uganda Schuhgeschäft Chinesische Händler
Picha: picture-alliance/AP Photo/S. Wandera

Wafanyakazi hao waliokasirika waliandamana nje ya ofisi za kampuni ya reli inayomilikiwa na China iitwayo Seventh Group katika mji mkuu, Kampala.

Mmoja wa wafanyakazi hao, Agnes Namusisi, alisema mameneja huwalipa wafanyakazi ambao "wanakubali vivutio vyao vya kutaka ngono".

Namusisi aliongeza kuwa yeye mwenyewe hajalipwa mshahara kwa muda wa miezi mitatu kwa sababu alikataa "kufanya mapenzi" na mkuu wake.

Madai hayo ya unyanyasaji yanajumuisha pia kufanyishwa kazi kwa masaa mengi na kipigo kutoka wasimamizi dhidi ya wafanyakazi wanaochelewa kufika  kazini.

Meya wa Kampala, Erias Lukwago, aliesema jiji hilo litatafakari kuiweka kampuni hiyo ya China katika orodha ya makampuni yasiyofaa, iwapo haitatatua matatizo ya wafanyakazi.