1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wagenknecht atangaza rasmi chama chake kipya Ujerumani

Saumu Mwasimba
9 Januari 2024

Mwanasiasa wa Ujerumani Sahra Wagenknecht aliyewahi kuwa kiongozi wa chama cha siasa za mrengo wa shoto, Die Linke, amezinduwa rasmi chama chake.

https://p.dw.com/p/4b1Dm
Mwanasiasa wa Ujerumani Sahra Wagenknecht
Mwanasiasa wa Ujerumani Sahra WagenknechtPicha: JOHN MACDOUGALL/AFP/Getty Images

Wagenknecht, aliyetangaza kujiondowa kutoka Die Linke mwaka jana, amesema chama chake cha Muungano wa Sahra Wagenknecht utatambuliwa kama chama cha wananchi nchini Ujerumani kwa miaka 30 hadi 40.

Kwa mujibu wa mwanasiasa huyo na wafuasi wake, chama hicho kinalenga kuleta mabadiliko ya kisiasa Ujerumani.

Kwa mujibu wa Wagenknecht, chama hicho kitawakilishwa katika chaguzi za bunge la Ulaya, lakini pia kinataka kusimamisha mgombea katika chaguzi za majimbo upande wa Mashariki mnamo mwezi Septemba mwaka huu.