1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUgiriki

Wahamiaji 100 waokolewa pwani ya Ugiriki

22 Julai 2023

Walinzi wa pwani wa Ugiriki wamewaokoa takriban wahamiaji 100 katika pwani ya nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4UGiP
Griechenland Kalamata Schiffsunglück Überlebende
Picha: John Liakos/AP Photo/picture alliance

Kulingana na kituo cha radio cha EPT kilichowanukuu walinzi wa pwani wa Ugiriki, wanaume watatu wanaoshukiwa kuwa walanguzi wa binadamu wamekamatwa.

Siku ya Ijumaa walinzi wa pwani waliripoti kwamba wahamiaji sabini na mmoja walipatikana katika boti ndogo karibu na mpaka wa kisiwa cha Karpathos walipokuwa waliekea Italy kutoka Uturuki.

Soma pia: Wahamiaji 300 hawajulikani waliko baharini Atlantiki

Watu wanaosafirisha binadamu kinyume cha sheria, mara kwa mara huwapitisha watu kwenye safari hatari ya baharini kutoka Uturuki na nchi za Afrika Kaskazini kuingia katika nchi wanchama wa Umoja Ulaya kama Ugiriki, Cyprus na Italia.