1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahandisi wa China waambiwa kuondoka Darfur

25 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CSqV

Chama cha waasi wa Darfur-JEM-kimeitaka Beijing ikiondoshe kikosi cha China kilichowasili Darfur kama sehemu ya ujumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika katika jimbo la Darfur.Saa chache tu baada ya kikosi cha wahandisi 130 wa Kichina kuwasili mji mkuu wa Darfur ya Kusini,Nyala chama cha JEM kilisema hakitowaruhusu wahandisi hao katika ardhi inayodhibitiwa na vikosi vyake.

Kiongozi wa JEM,Khalil Ibrahim amesema,China haishughuliki na haki za binadamu bali inavutiwa na malighafi ya Sudan.Chama cha JEM kimeilaumu Beijing kuwa inachochea mgogoro wa Darfur kwa kuisaidia serikali ya Khartoum.