1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahariri waitaka China ijali haki za binadmu

Abdu Said Mtullya9 Mei 2012

Wahariri wanazungumzia juu ya mkasa wa mpinzani asiyeona nchini China, kampeni ya uchaguzi nchini Marekani na juu ya soko la ajira nchini Ujerumani.

https://p.dw.com/p/14obl
Mpinzani,Chen Guangchen
Mpinzani, Chen GuangchengPicha: picture-alliance/dpa

Juu ya mpinzani wa China, Chen Guangcheng Gazeti la "Berliner Zeitung" linasema kama jinsi iliyvokuwa kwa mpinzani mwengine ,Ai Weiwei,au mshindi wa nishani ya amani ya Nobel Liu Xiaobo serikali ya China, kwa mara nyingine imeshindwa kuitumia fursa ya kutoa mfano wa utawala wa kisheria.

Gazeti hilo linaeleza kwamba hiyo ni ishara ya kusikitisha kwamba watetezi wa mageuzi, na wanasiasa wenye mrengo wa ukadirifu hawana sauti nchini China. Linasema ,mamlaka yamo katika mikono ya wanasiasa wenye mrengo mkali wanaohakikisha kwamba chama cha kikomunisti wakati wote ndicho kinachokuwa sahihi

.Gazeti la "Kölner Stadt Anzeiger" linapima kazi aliyoifanya Rais Obama mpaka sasa, hasa baada ya kufanya  ziara nchini Afghanistan. Gazeti hilo linasema Obama aliingia Afghanistan katika hali ya kiza kiza, lakini alipowahutubia watu wake palikuwa na mwangaza. Obama aling'ara kwenye televisheni na alitanda katika ukurasa wa Facebook:

Kwa kufanya ziara nchini Afghanistan Obama alilitekeleza jukumu analostahili kulitimiza wakati huu, yaani la kampeni ya uchaguzi. Hivi karibuni tu wajihii wake uliashiria ushaibu na hali ya wasi wasi. 
Hali halisi inamkabili Obama.Uchumi wa  nchi haujasimama dede.Usuluhishi wa  mgogoro wa Mashariki ya Kati umemponyoka. Jukumu la Afghanistan bado halijakamilika kabisa. Yumkini ziara ya Afghanistan imemwinua. Lakini ili kumshinda Mit Romney Obama atahitaji ziara nyingi kama hizo.

Gazeti la "Sächsiche Zeitung" linazungumzia juu ya soko la ajira nchini Ujerumani. Linasema idadi ya wasiokuwa na ajira imepungua nchini Ujerumani lakini mhariri wa gazeti hilo anatahadharisha kwa kusema kwamaba idadi ya wasiokuwa na kazi imepungua. Mnamo mwaka 2005 Wajerumani milioni tano hawakuwa na ajira, lakini leo ni chini ya milioni tatu. Hata hivyo hesabu hiyo inawajumuisha   wafanyakazi wa muda na wa mikataba mifupi, na malipo ya chini sana. Hiyo inaweza kuwa bahati ya kuazima. Mhariri anasema pamoja na haja ya kuleta myumbuko katika soko la ajira, haitakuwa sawa kutetea kazi za mishahara ya chini.

Gazeti la "Westdeutsche Zeitung" linazungumzia juu ya wasi wasi wa Wajerumani juu ya waislamu wa madhehebu ya salafia. Mhariri wa gazeti hilo anasema mirengo  ya itikadi kali inatoweka mbele ya ufahamu mkubwa tu. Watu wanapaswa kujua kwamba chuki na laghai zinasababisha mvutano. Lakini ikiwa waislamu na watu wengine kadhalika nchini Ujerumani wataingia katika mdahalo wa kuleta stahamala, tanga la wasalafia litatoka upepo.

Mwandishi:Mtullya Abdu/Deutsche Zeitungen.

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman