1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahariri wamsifu Rais mpya Gauck

Abdu Said Mtullya20 Machi 2012

Rais mpya wa Ujerumani Joachim Gauck leo anaanza kuutumikia muhula wa kwanza wa wadhifa wake. Wahariri wa magazeti wanatoa maoni yao juu ya Rais huyo anaetokea Ujerumani Mashariki.

https://p.dw.com/p/14Ml7
Rais mpya wa Ujerumani Joachim Gauck(Kulia) aanza kazi
Rais mpya wa Ujerumani Joachim Gauck(Kulia) aanza kaziPicha: dapd

Mhariri wa gazeti la "Nordsee" anasema mwitikio mkubwa kutoka ndani na nje juu ya kuchaguliwa Joachim Gauck unathibitisha jinsi anavyostahili kuutumikia wadhifa huo.Ni matumaini ya kila mtu kwamba atafanikiwa katika kazi yake, hasa kwa kuyazingatia yaliyotokea hivi karibuni katika ofisi ya Rais.

Mhariri wa gazeti la"Cellesche" anasema Rais Joachim Gauck hatakuwa msema ndio tu, wakati wote lakini ni mtu mwenye uwezo wa kuwa Rais wa dhati atakaezigusa nyoyo za wananchi. Mhariri wa gazeti la "Cellesche" anaeleza kuwa Rais Gauck atapaswa kuizingatia misingi anayoitetea. Katika kazi yake mpya atapaswa kuwa zaidi ya kasisi, anaetoa taarifa juu ya harakati za kupigania uhuru.Ingawa sifa hiyo anayo,jambo ambalo wajerumani wanalitaka sana. Gauck anao uwezo wa kuwa Rais mwema, wa dhati, atakaezigusa nyoyo za wananchi.

Kwa tathmini ya haraka mtu anaweza kusema ni sudi ya kihistoria kwamba Bwana Gauck anaetokea Ujerumani Mashariki amekuwa Rais wa Ujerumani wakati Kansela Angela Merkel pia anatokea huko huko. Lakini mharri wa gazeti la "Landeszeitung" anasema hayo ni matokeo ya historia, na anafafanua kuwa Wajerumani wa magharibi wamekulia katika mfumo wa kibepari unaothamini uhuru wa kila mtu binafsi.Wajerumani wa Mashariki waliishi katika mfumo ulioubana uhuru wa mtu. Hata hivyo uvimbe uliojitokeza katika mfumo wa ubepari umesababisha uroho wa mabenki. Mwananchi wa kawaida ndiye sasa anaelipia uroho huo. Kwa hivyo pana hisia za mshikamano. Wananchi wanataka siasa za ukweli na za uadilifu. Gauck na Merkel wanayawakilisha maadili hayo.

Gazeti la " Ludwigsburger Kreiszeitung" linatilia maanani kwamba Bwana Gauck amechaguliwa muda mfupi baada ya Rais wa hapo awali Christian Wulff kujiuzulu kutokana na tuhuma za kuhusika na kashfa. Kwa hivyo sasa Bwana Gauck analo jukumu la kuirejesha imani ya Wajerumani juu ya wadhifa wa Urais.

Mhariri wa gazeti hilo anasema Gauck anapaswa kufanikiwa katika jambo moja, kwamba anapoitazama ofisi ya Rais,mwananchi asianze kufikiria juu ya kuondoka ghafla kwa Rais wa hapo awali na juu ya malipo makubwa atakayopewa Bwana Wulff. Pamoja na hoja zote zinazotolewa juu ya malipo ya Rais, sasa Ujerumani imamhitaji Rais atakaeirejesha imani ya wananchi juu ya wadhifa wa Rais.

Mhariri wa gazeti la "Westfalen Blatt" anattilia manani kwamba Bwana Gauck atajenga mawasiliano na pande zote, kwa yeye hayumo katika chama chochote cha kisiasa. Lakini ni wazi kwamba hatakuwa na msimamo wa kuvipinga vyama. Atawapa matumaini Wajerumani wengi kwa sababu wanamwamini. Katika dakika sita za hotuba yake Joachim Gauck aliziamsha hisia za furaha.

Mwandishi: Mtullya Abdu/Deutsche Zeitungen/

Mhariri:Abdul-Rahman