1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waingereza waunga mkono Brexit

24 Juni 2016

Wananchi wa Uingereza wamepiga kura ya maoni iwapo nchi ibakie au ijiondoe kwenye Umoja wa Ulaya. Mchuano ulikuwa mkali matokeo yanaonyesha Brexit yashinda.

https://p.dw.com/p/1JCHR
Mshangao na fadhaa baada ya matokeo ya kura ya maoni ya Uingereza kutangazwaPicha: Getty Images/R. Stothard

Waingereza waamua kuachana na Umoja wa Ulaya."Ni siku ya huzuni kwa Ulaya anasema waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier.

Ripoti za asubuhi hii kutoka Uingereza ni za kuvunja moyo "Ni siku ya huzuni kwa Ulaya na kwa Uingereza" ameandika kwa lugha ya kiingereza waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani katika mtandao wake wa Twitter.

Katika taarifa yake kwa njia ya televisheni,spika wa bunge la Ulaya, Martin Schulz amesema kwa upande wake atakutana na kansela Angela Merkel ili kujadiliana namna ya kuepusha mfululizo wa majibu yanayotokana na kura ya Brexit ya Uingereza.

"Majibu ya kuvunja moyo kutoka kwa wale wanaoupinga Umoja wa ulaya wanaoshrehekea hivi sasa hayatotokea" amehakikisha mwanasiasa huyo wa chama cha Social Democratic cha Ujerumani.

"Sijashangaa,tulikuwa tumejiandaa" ameongeza kusema spika huyo wa bunge la Ulaya, Martin Schulz.

Ulaya yasaka njia ya kuepusha kishindo

Mwenyekiti wa vyama vya kihafidhina katika bunge la Ulaya, Manfred Weber amesema matokeo ya kura ya maoni ya Uingereza yatakuwa na madhara kwa pande zote mbili-Uingereza na Umoja wa Ulaya pia.

Deutschland Bundestag Berlin - Außenminister Frank-Walter Steinmeier
Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Frank-Walter SteinmeierPicha: picture-alliance/dpa/S. Kembowski

Ufaransa pia imeelezea masikitiko yake na kukumbusha Ulaya inabidi ijibu ili irejeshe imani ya wananchi.

Waingereza wamepiga kura kujitoa katika Umoja wa Ulaya. Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa hivi punde asili mia 52 ya wapiga kura wameamua nchi yao ijitoe katika Umoja wa ulaya.

Masoko ya hisa yaparaganyika

Kura ya maoni ya Brexit imekuwa chanzo cha kupazwa sauti Scottland kuitishwa kura nyengine ya maoni ya kudai uhuru.Asili mia kubwa ya wakaazi wa Scottland wamepoika kura kusalia katika Umoja wa ulaya.

Großbritannien EU-Referendum Brexit
Nembu ya kuachana Uingereza na Umoja wa Ulaya-BrexitPicha: Reuters/N. Hall

Masoko mashuhuri ya hisa yanaashiria kuporomoka kwa karibu asili mia 10 yalipofunguliwa.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir

Mhariri:Andrea Schmidt