1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waislamu Ethiopia wapinga mahakama za Kiislamu za Somalia

6 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCm1

Jamii ya Waislamu nchini Ethiopia hii leo imetangaza kuwa inaunga mkono msimamo wa nchi yao kuhusu mahakama za kiislamu zinazosimamia baadhi ya maeneo katika nchi jirani ya Somalia.

Kiongozi wa kundi hilo muhimu la waislamu walio na msimamo wastani wanakashifu mahakama za muungano za kiislamu kwa kutangaza vita dhidi ya wakristo wa Ethiopia na kueneza misimamo mikali vilevile uhasama na ugaidi.

Anaongeza kuwa ghasia zilizotokea mwezi Septemba na Oktoba kati ya Wakristo na Waislamu magharibi mwa Ethiopia zilisababishwa na kundi la watu 500 waliopata mafunzo nchini Somalia.

Waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi ametangaza kuwa nchi yake iko tayari kwa vita na mahakama hizo za kiislamu na hoja hiyo kuidhinishwa na bunge kwa minajili ya kulinda nchi yake.Hata hivyo Ethiopia inakanusha madai kuwa imepeleka maelfu ya majeshi ya vita kuunga mkono serikali ya Somalia.Badala yake inakubali kuwa imepeleka washauri wa kijeshi