1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wajerumani wahofiwa kutekwa nyara Afghanistan

19 Julai 2007

Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani inatuhumu kuwa wananchi wawili wa Ujerumani wasiojulikana walipo,wametekwa nyara nchini Afhganistan.

https://p.dw.com/p/CB2f
Afghanistan
AfghanistanPicha: AP

Wizara hiyo imesema kuwa inajitahidi kupata habari zaidi juu ya watu hao.Lakini polisi ya Afghanistan imesema watu
hao waliokuwa wanafanyakazi kwenye kampuni moja mjini Kabul wametekwa nyara pamoja na dereva na mkalimani.

Habari zinasema kuwa wajerumani hao pamoja na wafanyakazi wao walikuwa katika barabara inayounganisha mji wa Kabul na wa Kandahar kusini mwa Afghanistan.Habari zaidi zinasema kuwa matilabani waliokuwa na silaha walilisimamisha gari la wajerumani hao katika barabara hiyo na kuwateka nyara.

Lakini msemaji wa matilabani bwana Zabihullah Mujahid amekanusha kuhusika na mkasa huo. Bwana Mujahid ameeleza kuwa amewasiliana na wapiganaji wote katika sehemu husika lakini hakuna anaejua lolote juu ya kutekwa nyara wajerumani hao.

Bwana Mujahid alisema hayo katika mahojiano ya simu na shirika la habari la Ujerumani DPA.

Hapo awali kulikuwa na habari kwamba wajerumani hao walikuwa katika ujumbe wa watazamaji katika jimbo la kati la Afghanistan.Lakini msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Ujerumani ameeleza kuwa wajerumani hao siyo watumishi wa Umoja wa Mataifa

Hadi sasa wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imeweza kuthibitisha tu, kuwa wananchi wawili wa Ujerumani hawajulikani walipo.

Msemaji wa wizara hiyo bwana Martin Jäger ameeleza ,kuwa kwa mujibu wa habari zilizopatikana wizara inaweza kutuhumu kuwa watu hao wametekwa nyara

Amesema wizara yake inawasiliana na ubalozi wa Ujerumani nchini Afghanistan ili kupata habari zaidi.

AM