1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wajerumani watatu wauwawa Afghanistan

Sekione Kitojo24 Juni 2009

Wanajeshi watatu wa Ujerumani waliokuwa katika doria waliuwawa jana baada ya kushambuliwa na wapiganaji wa Taliban nchini Afghanistan.

https://p.dw.com/p/IY6k
Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung akizungumzia kuuwawa kwa wanajeshi watatu wa Ujerumani wakati akizungumza na waandishi habari katika uwanja wa ndege wa Frankfurt.Picha: AP

Wanajeshi watatu wa Ujerumani waliokuwa katika doria karibu na eneo la Kunduz waliuwawa jana baada ya kushambuliwa na kundi la wapiganaji wa Taliban waliokuwa na silaha za kawaida pamoja na silaha za kupambana na vifaru. Waziri wa ulinzi Franz Josef Jung ameendelea hata hivyo kuunga mkono juhudi za kuleta hali ya utulivu katika eneo la kaskazini mwa Afghanistan.


Katika kikosi kinachofanya kazi za ujenzi mpya katika jimbo la Kunduz bendera zinapepea nusu mlingoti. Kutokana na kuuwawa kwa wanajeshi watatu wa Ujerumani kutoka katika jeshi la kimataifa la ulinzi wa amani ISAF, idadi sasa imepanda na kufikia 35. Wanajeshi hao , ambao wameuwawa walikuwa katika operesheni ya pamoja pamoja na wenzao wa Afghanistan, wakati kikosi chao kilichokuwa kikifanya doria kiliposhambuliwa siku ya Jumanne asubuhi, kiasi cha kilometa sita kutoka katika eneo la Kunduz ambako kikosi cha Ujerumani kinachoshughulikia ujenzi mpya kina makao yake.

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung atafahamishwa kuhusu shambulio hilo wakati akihudhuria luteka ya jeshi la majini.

Wanajeshi watatu wa jeshi la Ujerumani amesema Jung kuwa wameuwawa wakati wakifanya doria katika jimbo la Kunduz.

Walikuwa wakifanya doria na ndipo magaidi wakiwa na silaha pamoja na silaha za kupambana na vifaru walipowashambulia, na katika mapambano hayo wanajeshi watatu waliuwawa.


wanajeshi 35 wa jeshi la Ujerumani hadi sasa wameuwawa nchini Afghanistan. Wiki mbili zilizopita wanajeshi wawili pia walijeruhiwa. Hali ya usalama katika eneo walipo wanajeshi wa Ujerumani imeendelea kuwa mbaya anasema waziri Jung.

Hali ya usalama katika jimbo la Kunduz imekuwa mbaya. Katika eneo hilo hali imeendelea kuwa mbaya , kutokana na matukio ya mashambulizi ya kushtukiza, na mapambano ya silaha. Hali hii ya mapambano ya silaha inatarajiwa kuendelea zaidi. na kama utaangalia ni silaha gani magaidi wanatumia, sio tu silaha za kawaida , bali hata silaha za kupambana na vifaru, na hapa utaona kwamba hali ya usalama katika eneo la Kunduz imekuwa mbaya.


Wakati huo huo wanajeshi wa Afghanistan wakisaidiwa na vikosi vya jeshi linaloongozwa na NATO wamevamia ngome ya kijeshi ya wapiganaji kusini mwa Afghanistan na kuuwa wapiganaji 23.

Wapiganaji waliouwawa katika mapambano hayo katika jimbo la kusini la Uruzgan jana Jumanne ni pamoja na kamanda wa eneo hilo wa Taliban , amesema general wa jeshi la Afghanistan Sher Mohammad Zazai.

Amesema kuwa ndege za kivita kutoka jeshi la NATO zilishiriki katika mapigano hayo katika eneo la Chinarto, ambalo liko karibu na mji mkuu wa jimbo hilo wa Tirin Kot.kamanda wa Taliban kwa jina la Mullah Isamaeel aliuwawa katika shambulio hilo.

Operesheni hiyo ni sehemu ya juhudi zinazofanywa dhidi ya wapiganaji ili kuwaondoa wanamgambo wa Taliban kutoka katika ngome zao kabla ya uchaguzi mkuu wa Afghanistan uliopangwa hapo August 20.

►◄

Mwandishi :Renne Barbara/ZR/Sekione Kitojo

Mhariri:M.Abdul-Rahman