1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakaguzi watoa taarifa baada ya uchunguzi nchini Uingereza

8 Agosti 2007

Ng'ombe katika mashamba mawili kusini mwa London waliambukizwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa miguu na midomo kutoka kwenye maabara iliyo karibu na mashamba hayo

https://p.dw.com/p/CB27
Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown
Waziri mkuu wa Uingereza Gordon BrownPicha: AP

Wakaguzi wa afya nchini Uingereza wamesema katika ripoti yao kwamba Ng’ombe walioambukizwa virusi vilivyosababisha ugonjwa wa miguu na midomo katika mashamba mawili kusini mwa London walivipata virusi hivyo kutoka kwenye maabara iliyo karibu na mashamba hayo.

Hiyo ni taarifa ya awali ya matokeo ya wakaguzi wa afya tangu kuzuka mkurupuko wa ugonjwa wa miguu na midomo nchini Uingereza.

Taarifa hiyo imesema kwamba uwezekano wa virusi hivyo kupeperushwa kwa upepo au kusambazwa kwa mafuriko yaliyoukumba mji wa London ni uzembe wa kibinadamu.

Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown amesema lazima maswali yote yaliyochomoza kwenye ripoti hiyo yapate majibu.

Mashamba ya wanyama yaliyoathirika yako karibu na maabara ya serikali na kampuni ya kibinafsi ya utafiti wa madawa.