1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakaguzi wazuru kampuni za utafiti wa madawa

6 Agosti 2007

Mkurupuko wa ugonjwa wa miguu na midomo nchini Uingereza umesababisha kuanzishwa uchunguzi dhidi ya kampuni ya utafiti wa madawa ili kutathmini chanzo cha ugonjwa huo unao waambukiza wanyama.

https://p.dw.com/p/CHjt
Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown
Waziri mkuu wa Uingereza Gordon BrownPicha: AP

Wakaguzi wa afya na usalama nchini Uignereza wamezuru kampuni ya utafiti wa mdawa kusini mwa mji wa England ili kutathmini chanzo cha virusi vinavyo sababisha ugonjwa huo wa miguu na midomo kwa wanyama.

Kampuni ya utafiti inayomilikiwa na serikali nchini Uingereza pamoja na kampuni moja ya kibinafsi bado zinafanyiwa uchunguzi huku mkulima ambae wanyama wake wameathirika na ugonjwa huo anataka kuondolewa lawama.

Mkulima huyo anadai kuwa hapaswi kulaumiwa kwani yaliyotokea sio makosa yake.

Wakaguzi wanatarjiwa kutoa taarifa yao katika muda wa siku moja au mbili kuhusu matokeo ya uchunguzi unaofanywa katika kampuni ya utafiti ya Pirbright iliyo kilomita tano kutoka shamba la Woolford lenye ng’ombe walioambukizwa na virusi hivyo vinavyosababisha ugonjwa wa miguu na midomo.

Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown anatarajiwa kuongoza kikao cha sita cha dharura kitakacho lenga kuepuka madhara zaidi hasa katika mzozo mwingine unao ikumba sekta ya kilimo nchini Uingereza.

Umoja wa Ulaya leo utaridhia marufuku ya usafirishaji wa mifugo, bidhaa za nyama na maziwa iliyowekwa kwa hiyari na serikali ya Uingereza.

Marufuku hiyo itazuia usafirishaji wa bidhaa hizo katika nchi zote 27 wanachama wa umoja wa Ulaya.

Takriban ng’ombe 120 wamechinjwa katika shamba la Woolford na katika mashamba mengine jirani kuepuka hatari ya mambukizi.

Msemaji wa wizara ya mazingira mjini London amesema ng’ombe wawili walipatikana wakiwa wameambukizwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa miguu na midomo.

Ugonjwa huo uawaaambukiza kwa haraka wanyama wenye kwato kama vile n’gombe, kondoo na nguruwe. Wanadamu hawaambukizwi ugonjwa huo.

Eneo la Pirbright linamilikiwa na serikali ya Uingereza kwa ushirikiano na kampuni za Marekani na Ufaransa.

Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown amesema serikali yake itachukuwa hatua za haraka kudhibiti ugonjwa huo.

Mkurupuko wa ugonjwa wa miguu na midomo ulisababisha kuuwawa mifugo milioni 7 mnamo mwaka 2001 nchini Uingereza.

Serikali ya Ungereza ilipata hasara ya pauni bilioni nane na kusababisha hali ngumu kwa wakulima, sekta za kilimo na utalii ziliathirika vibaya mno takriban wanyama milioni kumi waliteketezwa.