1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakamatwa wakitaka kuzamia ulaya

18 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCiT

Istanbul. Polisi nchini Uturuki inawashikilia watu 254 wakiwemo wasomali, wairaq, wapalestina na wayemen wanaotaka kuingia barani Ulaya.

Watu hao walikamatwa katika hoteli moja mjini Istanbul wakiwa na nia ya kuingia ujerumani kupitia Italia kwa njia ya bahari ambapo hivi sasa wanasubiri kufunguliwa mashataka.

Polisi pia imemmakata meneja wa hoteli hiyo pamoja na watu wengine kadhaa kuhusiana na njama hizo za kusafirisha wahamiaji haramu barani Ulaya.

Kukamatwa kwa watu hao, kumekuja huku leo ikiwa ni siku ya wakimbizi duniani.