1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakenya wajiandaa kwa ujio wa Papa

Alfred Kiti24 Novemba 2015

Maandalizi ya kumpokea kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis, yamekamilika Kenya, huku wanananchi wakiwa na hamu kubwa kumuona Baba Mtakatifu huyo ambaye ni mara ya kwanza kuzuru Afrika.

https://p.dw.com/p/1HBvA
Kenia Papstbesuch Plakat in Nairobi
Picha: DW/D. Pelz

Siku ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu imewadia, Waumini wa dhehebu la Katoloki wanayo hamu kubwa ya kumuona kiongozi wao Baba mtakatifu Papa Francis anayetarajiwa kuwasili leo jioni mjini Nairobi kutoka Makao makuu ya Vatican. Ajenda kuu ya ziara yake Papa Francis ni kuhubiri amani na utangamano. "Ninakuja kama mtume wa injili kuutangaza upendo wa Yesu Kristo na ujumbe wake wa upatanishi, msamaha na amani.”

Kuambatana na ujumbe wa Baba Mtakatifu, Serikali ya Kenya imetenga siku ya Alhamisi tarehe 26 Novemba kuwa siku ya mapumziko ambapo wananchi watajiunga na misa itakayoongozwa na Papa Francis katika uwanja wa chuo kikuu cha Nairobi. Zaidi ya waumini milioni moja unusu wanatarajiwa kuwasili Nairobi kuhudhuria misa hiyo.

Papa kuzungumzia ulinzi wa mazingira

Kanisa la Holy Family Nairobi ambapo Papa atafanya misa
Kanisa la Holy Family Nairobi ambapo Papa atafanya misaPicha: DW/D. Pelz

Usalama umepewa kipaumbela na hakuna mtu atakayeruhusiwa kuingia katika uwanja huo ikiwa jina lake halipo kwenye orodha ya walijiosajili kuhudhuria. Atakapowasili katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta mwendo wa saa 12 jioni, Papa Francis atalakiwa kwa sherehe za nyimbo za wanakwaya na densi kisha msafara wake utafululiza hadi Ikulu ya Rais kulingana na taarifa yake msemani wa Ikulu ya Rais, Manoa Esipisu anasema: "Kutakuwa na sherehe za kumkaribisha katika uwanja wa ndege kama inavyoptarajiwa. Kutakuwa na graride la heshima katika ikulu ya Nairobi na kasha kufuatiwa na hituba za Baba Mtakatifu na Rais katika uwanja wa Ikulu.”

Mbali na kuhudiri amani na utangamano, Baba Mtakatifu anatarajiwa kuzungumzia swala zito la mabadiliko ya tabianchi ndio mana siku ya ijumaa atazuru makao makuu ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP huko Gigiri ambako atakutana na maafisa wa Kibalozi.

Papa Francis akiwa ni mpenzi watoto na vijana kwenye ratiba ya ziara yake amepangiwa kukutana na vijana katika katika uwanja wa michezo wa kasarani ambako atahitimisha ziara yake na kuondoka jioni kwenda uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta kuelekea nchini Uganda kumalizia ziara yake ya bara la Afrika