1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakimbizi wa darfour wanataka wanajashi wa kimataifa wapelekwe haraka

18 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBXz

“Tume ya pamoja ya Umoja wa mataifa na umoja wa Afrika inabidi iingilie kati haraka” –wanasemas hayo wakaazi wengi wa Darfour waliolazimika kuyahama maskani yao ili kuyanusuru maisha yao.Wengi wao wanaamini pekee kikosi hicho cha pamoja ndicho kitakachoweza kulinda amani na kudhamini kurejea kwao majumbani mwao.”Hakutakua na amani bila ya wanajeshi wa kimataifa” amesema hayo Ahmed Hirs a naeishi katika kambi ya wakimbizi ya Otash,kaskazini mwa mji wa Nyala.Katika kambi hiyo wanaishi wakimbizi 62 elfu wemngine waliokimbia mauwaji,ubakaji na uporaji.Kikosi cha pamoja na Umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika kitakachokua na wanajeshi 26 elfu,kinatazamiwa kupelekwa Darfour mwakani.Wakimbizi wanalalamika wakihoji huo ni muda mrefu mno.