1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakimbizi waandaliwa sherehe za Krismasi Ujerumani

Mjahida24 Desemba 2015

Makundi yakujitolea yaandaa sherehe za krismasi katika makambi ya wakimbizi nchini Ujerumani. Lengo la shughuli hii ni kutoa uelewa wa tamaduni za wajerumani kwa wakimbizi hao wapya na pia kutoa zawadi kwa watoto wadogo.

https://p.dw.com/p/1HTNa
Troisdorf Weihnachtsfest in Flüchtlingsunterkunft
Picha: www.conrady.net

Mkesha wa Kristmasi au "Heiligabend" kwa kijerumani ni shughuli ambayo watu wengi nchini Ujerumani wanaisherehekea wakiwa na familia, marafiki yani kuja pamoja na kugawana na wasionacho.

Hii ndio maana makundi mengi ya kujitolea yakaamua kutumia krismasi kama nafasi muhimu ya kuwaleta wakimbizi pamoja na kutoa zawadi kwa watu hawa wanaoomba uhifadhi.

Mjini Bonn, kijana Adelina Müller aliye na miaka 24 akiwa pamoja na rafiki yake Pia Püschel waliandaa tukio kwa jina "Krismasi ndani ya boksi la viatu" walilolifanya katika kambi ya wakimbizi ya Ermekeilkaserne inayowapa hifadhi wakimbizi takriban 500 kutoka mataifa kama Syria, Afghanistan, Iran na Iraq.

Watoto wakitazama zawadi zao katika tukio la "Krismasi ndani ya boksi la viatu"
Watoto wakitazama zawadi zao katika tukio la "Krismasi ndani ya boksi la viatu"Picha: Adelina Müller

"Tuliomba watu watusaidie na michango, tukanunua zawadi na kuzipaki vizuri, tulikuwa karibu sana na watoto ambao tuliwafundisha lugha ya kijerumani katika kambi hiyo," alisema Müller alipozungumza na DW. Ameongeza kuwa waligundua watoto hao wanahitaji kutunzwa zaidi, kwahiyo walitaka tu kuwafurahisha.

Watoto waliyopokea zawadi zilizokuwa zimefungwa katika maboxi ya viatu walifurahi, alisema mwalimu huyo kijana wa lugha ya kijerumani.

Amesema kitu kilichowashangaza ni kwamba hawakufungua maboksi yao haraka, walitaka kufanya hivyo wakati watakaporejea katika vyumba vyao.

Makundi ya kujitolea yasema changamoto kubwa nikuwafurahisha wakimbizi

Kwake Olaf Conrady, mpiga picha wa kujitolea katika kambi ya wakimbizi ya Troisdorf, iliyoko karibu na mji wa Bonn, sherehe za krismasi ni njia moja ya kujumuika na wahamiaji wanaosubiri visa zao na mpango wa muda mrefu wa kuishi katika eneo wanaloomba hifadhi.

"Moja ya chanamoto kubwa ni kuwafurahisha wakimbizi, tuliwapa biskuti, keki na vinywaji visivyokuwa na mvinyo, kwasababu wakimbizi wengi katika kambi hiyo walikuwa waislamu," alisema Conrady.

Tukio hilo lilikuwa na mziki kutoka maeneo yote, nyimbo za krismasi, nyimbo za kitamaduni, za kileo, watu walikula, wakacheza pamoja na hata kuwa na densi za kitamaduni.

Wakimbizi hao huenda wakajiskia wamekaribishwa nchini Ujerumani iwapo pendekezo la muakilishi wa tamaduni nchini Ujerumani, Aydan Özuguz kwamba kuwepo na maandishi ya kiarabu yanayoelezea kinachosemwa katika hotuba ya krismasi na mwaka mpya ya Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa Ujrumani Joachim Gauk.

Wanaume wakijumuika pamoja katika kambi ya wakimbizi ya Troisdorf
Wanaume wakijumuika pamoja katika kambi ya wakimbizi ya TroisdorfPicha: www.conrady.net

Muakilishi huyo pia aliomba kuwepo na maandishi sawa na hayo kwa lugha ya kipersha, Pashto, Kingereza na Kifaransa.

Takriban wakimbizi milioni moja wanaokimbia umasikini na mapigano Mashariki ya Kati pamoja na Afrika wamewasili nchini Ujerumani tangu mwazoni mwa mwaka huu. Ongezeko la wakimbizi hata hivyo limesababisha maandamano kutoka kwa makundi ya mrengo wa kulia, lakini pia kumekuwepo na ukarimu kutoka kwa baadhi ya raia wa Ujerumani.

Mwandishi: Amina Abubakar/DW

Mhariri:Iddi Ssessanga