1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakimbizi wakirundi wauwawa DRC

Saumu Mwasimba
16 Septemba 2017

Wakimbizi wasiopungua 18 wauliwa na jeshi DRC.Idadi hiyo ni ya awali iliyotolewa ingawa huenda ikaongezeka

https://p.dw.com/p/2k5yJ
Kongo Lusenda MONUSCO Flüchtlingslager burundische Flüchtlinge
Kambi ya Lusenda-Kivu KusiniPicha: MONUSCO/Abel Kavanagh

Wanajeshi wa Congo wamewapiga risasi na kuwauwa wakimbizi 18 wakiburundi kufuatia mapigano yaliyozuka katika eneo la Kamanyola mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.Hayo yameelezwa na maafisa wa eneo hilo katika mkoa wa Kivu Kusini na kutowa idadi hiyo ya awali ambayo huenda ikawa zaidi.Mkimbizi mmoja wa kiburundi amesema kwamba zaidi ya 30 wameuwawa na wasiopungua 100 wamejeruhiwa.

Afisa mmoja kutoka wizara ya mambo ya ndani Josue Boji amesema wanajeshi walijaribu kuwatawanya wakimbizi kwa kufyetua risasi hewani lakini walizidiwa nguvu baada ya kundi kubwa la wakimbizi kuivamia jela inayosimamiwa na shirika la ujasusi wa ndani wakitaka waburundi wanne wanaoshikiliwa katika jela hiyo waachiwe huru.

Burundi Flüchtlinge
Picha: Reuters/T. Mukoya

Inatajwa kwamba idadi ya awali inaweza ikaongezeka kutokana na wakimbizi hao kuzitwaa baadhi ya maiti za watu wengine waliouwawa na kuzipeleka katika kambi ya Umoja wa Mataifa inayosimamiwa na wanajeshi wa Pakistan katika eneo la Kamanyola.Msemajai wa ujumbe mkubwa wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa MONUSCO nchiniCongo pia alitoa idadi ya awali ya waliouwawa kuwa ni wakimbizi 18 na 50 wamejeruhiwa.

Mkimbizi mmoja akieleza juu ya tukio hilo ameliambia shirika la habari la AFP kwamba ameshuhudia watu wakianguka chini waume,wanawake na watoto ambao walikuwa hawana silaha ya aina yoyote,na ameeleza kuona maiti 31 na wengine wasiopungua 105 wakiwa na majeraha.Malefu ya warundi walikimbilia DRC kuepuka wimbi la mashambulio na vurugu  zilizoikumba nchi yao mwaka 2015 baada ya rais Pierre Nkurunzinza kuamua kugombea tena madaraka.Kuna kiasi warundi 36,000 wanaoishi DRC wengi wakiwa katika kambi yenye msongamano ya Lusenda Mashariki mwa nchi hiyo.

Mwandishi:Saumu Mwasimba

Mhariri:Sudi Mnette

Source:afp