1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakimbizi wanasa mpakani Italia

18 Aprili 2011

Italia imefanya kile ilichotishia kutenda - imetoa vibali vya muda vya usafiri kwa wakimbizi waliotokea Afrika ya Kaskazini.

https://p.dw.com/p/RIaO
epa02678674 A boat with immigrants on board arrives on the Italian island of Lampedusa, southern Italy, on 09 April 2011. Reports state that Italy and France agreed on 08 April 2011 to carry out joint patrols of the Tunisian coast to block migrants headed for Europe, with the French interior minister saying there was no duty to take in boat people. EPA/ETTORE FERRARI
Wakimbizi waliowasili kisiwani Lampedusa,ItalitaPicha: picture alliance/dpa

Italia imechukua hatua hiyo kwa sababu inahisi kuwa haipati msaada wowote kutoka nchi wanachama wenzake wa Umoja wa Ulaya kukabiliana na wimbi la wakimbizi kutoka kaskazini mwa Afrika. Vibali hivyo vya usafiri vya muda wa miezi sita, kimsingi vinawaruhusu wakimbizi hao kuingia katika nchi za Umoja wa Ulaya zilizotia saini mkataba wa Schengen, unaowaruhusu wasafiri kuvuka mipaka ya nchi hizo bila ya kukaguliwa.

Lakini Ufaransa katika jitahada ya kuzuia wimbi hilo la wakimbizi, imetoa masharti mapya - wenye vibali hivyo vya muda wanahitaji kuwa na ushahidi kuwa wanaweza kulipia gharama zao. Kwa hivyo, licha ya kumiliki vibali vya usafiri, ni wakimbizi wachache tu walioweza kuvuka mpaka na wamekusanyika katika kambi iliyofurika kwenye mji wa Italia Ventimiglia ulio mpakani na Ufaransa. Wengi wa wakimbizi hao wametokea Tunesia na lengo lao kuu ni kuingia Ufaransa. Lakini hiyo jana, Ufaransa ilizuia kwa muda mrefu, usafiri wa treni kutoka Ventimiglia.

Tatizo la wakimbizi lazusha mvutano wa kidiplomasia

Franco Frattini, the Italian Foreign Minister in Tirana declaring on visa liberalization for Albania and Bosnia- Herzegovina.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia Franco FrattiniPicha: AP

Wakimbizi hao walionasa mpakani, waliungwa mkono na makundi ya wanaharakati wa haki za binadamu walioandamana kwa ghafula, hadi kwenye ofisi ya ubalozi wa Ufaransa iliyo karibu na kituo cha treni, lakini polisi ilizuia ghasia kuibuka. Hali iliyozuka mpakani, imesababisha mvutano wa kidiplomasia kati ya Italia na Ufaransa.Waziri wa mambo ya nje wa Italia Franco Frattini amelalamika rasmi kuhusu vikwazo vya usafiri wa treni. Wakati huo huo waziri wa ndani wa Italia Roberto Maroni amekosoa vikali msimamo wa nchi wanachama wenzake wa Umoja wa Ulaya, wa kutoisaidia vya kutosha kukabiliana na tatizo la wakimbizi wa Afrika ya Kaskazini.

Italy's Minister of Interior Roberto Maroni gives a press conference in Catania, February 15 2011. Maroni said migrants who have landed on the island of Lampedusa threaten the institutional and social structures of Europe and that Italy was asking the EU for euros 100million to tackle the influx. EPA/ORIETTA SCARDINO +++(c) dpa - Bildfunk+++
Waziri wa mambo ya Ndani wa Italia, Roberto MaroniPicha: AP

Wakimbizi wenye vibali waruhusiwe kusafiri

Waziri Maroni alisema kuwa wao wamechukua hatua kuambatana na sheria za Ulaya na wakimbizi hao wamepatiwa vibali vya usafiri na hati zingine zote zinazohitajiwa. Akaongezea kuwa hiyo imetambuliwa pia na Halmashauri ya Umoja wa Ulaya. Watunisia wengi waliopata vibali na hati za usafiri sasa ndio wamekusanyika Ventimiglia na hata kwenye kituo cha treni, wakitazamia kuwa hatimae, ndoto yao ya kuingia Ufaransa itakuwa ukweli.