1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vyakula vya njee mjini Kinsasha

16 Februari 2017

Katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, migogoro inaendelea na hali ya uchumi inazidi kuwa mbaya.Watu wengi sasa wasioweza kumudu maisha, wamelazimika kula njee sehemu za bei rahisiza vyakula vya nje yaani Mama ntilie

https://p.dw.com/p/2XhmP
Kongo Fluss Markt
Wauzaji chakula karibu na kijiji cha Ngamanzo, jimbo la KinshasaPicha: Getty Images/AFP/J. Khanna

Joseph Magamba, muendesha taxi mweenye umri wa miaka 29, anasema anaweza kula kwa chini ya faranga  2000 ( ambazo ni sawa na euro 1 ), katika sehemu zinazouza vyakula njee au mama ntilie. Joseph anayaelezea hayo huku akiwa na sahani ya chuzi zito la kuku, ambayo alilipia faranga 1,500, na pembeni kuongezea fufu, chakula kinachofanana na ugali , kwa faranga 400. Kijana huyo anasema kwamba katika hoteli ya kawaida angalilazimika kuingia gharama mara kumi zaidi ili kupata mlo kama huo kitu ambacho anakiri hawezi kumudu.

Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imekuwa ikikabiliwa na migogoro ya kiuchumi na kisiasa kwa miaka mingi, kitu ambacho kimesababisha kushuka kwa kiwango cha uzalishaji na kupanda kwa gharama ya maisha baada ya kushuka thamani sarafu  ya nchi hiyo .

Pia raisi wa nchi hiyo kukataa kukabidhi madaraka Desemba mwaka jana kumezidi kuchangia mgogoro wa kisiasa kuwa mbaya zaidi nchini humo.

Magenge ya wauza chakula au mama ntilie yamezidi kupata umaarufu mwaka mmoja na nusu uliopita mjini Kinshana, na sio tu kwa watu wanotafuta malaji ya urahisi lakini pia kwa wanawake wa nyumbani kama vile Marie Aloko Hioma, ambao pia wameanza kuuza vyakula vilivyopikwa mbele ya nyumba zao mjini Kinshasa.

Demokratischen Republik Kongo - Stau in der Hauptstadt Kinshasa
Mjini Kinshasa ambapo watu wengi sasa huponea vyakula vya kupikwa njee.Picha: DW/D. Köpp

Akina mama wengi waingia katika biashaya ya kuuza chakula

Mama Marie mwenye watoto  wanane , alisema  ameanzisha sehemu hii ya kuuza chakula, mama ntilie, miaka sita iliyopita ili kuweza kulipia ada za  shule ya watoto wake.

 Asubuhi saa kumi na moja  kila siku, watu huanza  kujitokeza hapo kwake ili kupata  samaki, kuku na pondu chakula cha kienyeji kilichotengezezwa na mboga ya muhogo na  mbogamboga nyengine.

Kwa uhakika  mama Marie hajui watu wangapi wanafika katika sehemu yake kwa siku

"Nakisia ni kama watu mia na kidogo," alisema

Kwa miaka saba pia Mama Annie amekuwa akifanya biashara  kama hiyo, karibu na hapo.  Mapato yake yeye anasema hutumia kwa ajili ya kununulia nguoa za watoto wake.

Mteja wake wa kila siku ni Papi Bula Mbemba mwenye umri wa miaka 49, naye anasema :

"Hapa unapata bei za kuridhisha. Sehemu hizi za vyakula  zinawapatia watu wa Kinshasa suluhu ya tatizo hili.

Suala la usafi katika sehemu za kula

Lakini juu ya yote hayo, vyakula hivi vya urahisi vinaambatana na wasiwasi wa suala la usafi. Muendeshaji taxi Bangamba anasema kuna baadhi ya wamiliki wa sehemu zinazo uza chakula, wanatumia sahani na gilasi zisizooshwa.

Wateja pia huwa hatarini kupata magojwa kama vile homa ya matumbo, kuharisha na hata pia cholera kwa vile sehemu hizi za vyakula vya nje nyingi huwa zipo katika mazingira machafu kama vile sehemu za majaa na mazingira ya maji machafu.

"Ugumu wa maisha unawafanya watu kula kile wanachoweza kumudu," alisema Benjamin Kewngani Mavard, mkuu wa usafi wa Uma. Akionya kuwa kutakuwa na ongezeko la tatizo la afya kwa Uma.

"Ni vigumu kuwafungia wauzaji chakula biashara zao," Aliongezea.

"Lazima wauzaji wazingatie usafi,"aliendelea kusema.

Mama Marie alisema japo kuwa wengine hawatimizi swali la usafi, sehemu yake yeye ni safi.

"Familia yangu na mimi tunakula kile ninachokipika," alisema huku akiosha vyombo vyake

huku pia akisistiza kwamba hataki  wateja wake wapate madhara.

Mwandishi : Najma Said

Mhariri :       Saumu Mwasimba