1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakurudi watoa ushahidi dhidi ya rais wa zamani wa Irak, Saddam Hussein

10 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD4E

Mashahidi wa kikurudi nchini Irak waliiambia mahakama kwamba utawala wa rais wa zamani wa Irak, Saddam Hussein, ulitumia matingatinga kuwazika wakiwa bado hai jamaa zao katika makaburi ya pamoja. Waliyasema hayo wakati kesi yake na washitakiwa wengine 6 kwa mauaji ya kuangamiza halaiki ya watu, ilipoanzishwa kusikilizwa tena jana mjini Baghdad baada ya kusitishwa kwa wiki kadhaa.

Saddam Hussein na watuhumiwa wengine, wanakabiliwa na mashitaka ya kukishambulia kijiji cha kikurudi cha Anfal kaskazini mwa nchi mnamo mwaka wa 1988 na kuwauwa watu zaidi ya 180,000. Wiki ijayo, ndipo inatarajiwa kutolewa hukumu dhidi ya Saddam Hussein juu ya kesi zilizotangulia kuhusu makosa dhidi ya binaadamu kwa mauaji ya Washiha 148 kufuatia jaribio la mauaji dhidi yake katika mji wa Dujail mnamo mwaka wa 1982.