1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakuu wa vyama vyote vya kisiasa nchini Irak watoa mwito makundi ya wanamgambo yapokonywe silaha

Hamidou, Oumilkher6 Aprili 2008
https://p.dw.com/p/Dcxh

Mosul:

Wanafunzi 42 waliotekwa nyara karibu na mji wa kaskazini wa Irak-Mosul wameachiwa huru.Vikosi vya usalama vya Irak vimewaokoa wanafunzi hao muda mfupi baada ya kutekwa nyara.Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Irak,watu waliokua na silaha waliyasimamisha mabasi mawili yaliyokua na wanafunzi wa chuo kikuu cha Mosul na kuwateka nyara.Wakati huo huo wakuu wa vyama vyote vya kisiasa vya Irak wamekutana mjini Baghdad hii leo na kuyatolea mwito makundi yote yawapokonye silaha wanamgambo  wao na wayavunje makundi hayo.Hilo ndilo sharti pekee la kuweza kuchangia katika utaratibu wa kisiasa na kuishiriki katika uchaguzi ujao nchini humo.Waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na rais Jalal Talabani ,waziri mkuu Nuri El Maliki na wakuu wa vyama vyote vinavyowakilishwa bungeni..