1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakwepa kodi wanasakwa nchi mbali mbali

27 Februari 2008
https://p.dw.com/p/DDvM

BOCHUM:

Kwa mujibu wa serikali ya Ujerumani,sasa Marekani,Australia,Italia na Sweden pia zinawasaka wakwepa kodi ya mapato kuhusu mkasa wa Liechtenstein.Hadi hivi sasa maafisa wa idara ya kodi nchini Ujerumani wamesaka nyumba za kama watu 150 kuhusika na madai kwamba hadi matajiri 1,000 wameficha pesa zao nchini Liechtenstein ili kukwepa kulipa kodi ya mapato.Washukiwa wengine 72 kwa hiyari wamejipeleka kwa waendesha mashtaka.

Idara ya Kodi za Ndani ya Marekani imesema,inawachunguza zaidi ya Wamarekani 100 waliokuwa na akaunti nchini Liechtenstein.Maafisa wa Australia pia wamesema,wanachungza kiasi ya kesi 20.